Na Mwandishi wetu - Mahakama
Wanamichezo wanaoshiriki mashindano ya Meimosi mkoani Morogoro jana tarehe 26 Aprili, 2023 ikiwa Siku ya Maadhimisho ya Miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar wamesherehekea sherehe hiyo kwa kutoa msaada wa mahitaji mbalimbali kwa vituo vinne vya watoto wanaoishi katika mazingira magumu kimoja cha na wazee.
Akizungumza baada ya kupokea msaada huo, Mkurugenzi wa Kituo cha Amani Centre kilichopo Fr. Beatus Martin Sewango amesema misaada kama hii inahitajika katika kituo hiki kutokana na kwamba watoto wanaolelewa katika kituo hiki ni wale wenye ulemavu wa viungo hivyo wanahitaji kupata vifaa vya mazoezi na pia kupata bima za afya ili kuweza kutibiwa.
Mkurugenzi huyo ametoa wito kwa wazazi na walezi kutowaficha watoto wenye ulemavu badala yake wajitokeze ili waweze kupatiwa msaada wa matibabu hasa mazoezi, “wazazi wamekua na tabia ya kuwaficha watoto wenye ulemavu na wengine kuwatelekeza kwa bibi zao ambao ni wazee hawawezi kuwahudumia waleteni hapa wapate wapate tiba na mazoezi maana wengi wamepona kupitia mazoezi na wanaendelea na masomo,” alisema.
Aidha aliwashukuru wanamichezo hao kwa upendo waliouonesha kuwatembelea watoto hao, na ameomba waendelee kuwatembelea na kutoa misaada maana kituo hicho hakina wafadhili zaidi tu ni vikundi vya watu kama vile wanamichezo, hivyo bado uhitaji ni mkubwa kutokana na changamoto za watoto wanaolelewa hapo wakiwa na ulemavu.
Wanamichezo hao wametembelea kituo cha kulelea watoto cha Amani Centre, Mwenda, Homeless,Lugono na kituo cha kulelea wazee cha Fugafuga vituo vyote hivi viko manispaa ya Morogoro.
Baada ya mapumziko hayo kesho mashindano yanaendelea kama kawaida katika viwanja vya Jamhuri katika ngazi ya nusu fainali ambapo timu ya mpira wa miguu na kamba wanaume wamefanikiwa kuingia fainali.
Baadhi ya wanamichezo wa Mahakama Sports wakijiandaa kupeleka mahitaji katika vitro via watt kenye mahitaji.
Baadhi ya mahitaji yöliyotolewa na wanamichezo hao.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni