Jumatatu, 10 Aprili 2023

MAHAKAMA YAIBUKA KIDEDEA MECHI ZA KIRAFIKI TABATA

Na Eunice Lugiana-Mahakama, Kibaha

Katika kuelekea mashindano ya Mei Mosi yanayotarajiwa kuanza tarehe 15 Aprili, 2023 mkoani Morogoro, timu za kamba wanawake na mpira wa miguu zimeibuka kidedea dhidi ya timu ya tabata veterany katika viwanja vya Sigara Tabata jijini Dar es salaam. 

Katika mchezo huo wa kirafiki, Mahakama imewafunga veterans magoli 2 kwa 1, wakati mchezo wa kuvuta kamba wanawake wa Mahakama wamewavuta wanaume wa Tabata veterany kwa awamu mbili. 

Akiongea na wachezaji baada ya pambano hilo, Mhazini wa Tabata veterans, Wakili Nasoro Katunga amewasifia Mahakama kwa kuwa na timu bora yenye nidhamu hasa kwa kutunza muda wa kufika mazoezini ukilinganishwa na wenyeji Tabata veterans ambao walichelewa kufika na kukuta Mahakama walishafika na kuanza mazoezi ya viungo. Amesema hiyo ni nidhamu nzuri katika michezo kwa kutunza muda. 

Aidha, kiongozi huyo amewasifia wachezaji wa kamba wanawake kwa kuonyesha umahili katika mchezo huo, hivyo kupelekea ushindi kwa awamu mbili. “Tunawapongeza sana wanawake wa Mahakama kwa kufanikiwa kutuvuta sisi wanaume, ni jambo ngumu mwanamke kumzidi nguvu mwanaume,” alisema. 

Katika pongezi zake hizo, amezitakia kila la heri timu zote za Mahakama zitakazo kwenda kushiriki mashindano ya Mei Mosi na kueleza kuwa kama juhudi zaidi ya hizo zikiongezwa makombe yote yatabaki mahakamani. 

Amemsifia kolikipa wa Mahakama, Mhe. Fahamu Kibona kuwa ni mzuri, hivyo kwake yeye nyota wa mchezo ni kolikipa huyo. Timu hizo za Mahakama ziko katika hatua ya mwisho ya maandalizi ya mashindano ya Mei Mosi.

 






 Kiongozi wa timu ya Tabata veterans, Wakili Nasoro Katuga akiongea na wachezaji wa timu ya Mahakama na timu ya Tabata veterans.

Golikipa wa timu ya Mahakama, Mhe. Fahamu Kibona aliyeibuka nyota wa mchezo kwa kudaka kwa umahili.

 Baadhi ya wachezaji wa timu ya Mahakama na Tabata veterans wakimsikiliza kiongozi wa Tabata veterans.

(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam).

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni