Ijumaa, 21 Aprili 2023

MAHAKAMA YAZIDI KUNYANYUA MABAWA MASHINDANO YA MEI MOSI

Na Evelina Odemba – Mahakama Morogoro

Timu ya mpira wa miguu kutoka Mahakama Sports Klabu imeichapa magoli matatu (3) kwa moja (1)  timu ya Wakala wa Uhifadhi wa Chakula (NFRA) katika mashindano ya kuwania kombe la mei mosi yanayoendelea Mkoani Morogoro.

Ushindi huo uliopatikana leo tarehe 21 Aprili, 2023 katika viwanja vya shule ya Sekondari Morogoro na katika mchezo huo Timu ya Mahakama ilihakikisha NFRA inaenda mapumziko ikiwa imetandikwa goli moja ambalo lilifungwa na Gabriel Tabana aliyemuhamisha kipa golini kuufuata mpira na hakubahatika kuhimili shuti kali kutoka kwa Tabana.

Aidha katika kipindi cha pili Mahakama iliizawadia NFRA magori mengine mawili na kufanya idadi ya magoli kwa upande wa Mahakama kuwa matatu (3) wafungaji wa goli la pili ni Martin Chertro Gizbert aliyeongeza goli lingine huku wakala wa chakula wakiambulia gori moja la kufutia machozi. 

Timu ya mpira wa miguu kutoka Mahakama tayari imecheza mechi nne za makundi na katika mechi hizo imefunga mechi mbili na kutoka sare ya sifuri katika mechi mbili (2) na imebakiza mechi moja kukamilisha hatua ya makundi wakati huo huo timu hii inatazamwa kama miongoni mwa timu kubwa na tishio katika mashindano hayo ya mei mosi.

Mashindano haya bado yanaendelea mkoani hapa na walimu wa timu zinazoshiriki toka Mahakama wameendelea kusisitiza kuwa watashinda kwa kishindo kwani wameshafanya vizuri kwa michezo iliyopita hivyo hawana hofu kuwakabili wapinzani wao katika michezo ijayo. Ushindi huu wa Mahakama umekuwa chachu ya wachezaji ambao kila kukicha wanajifua kukabiliana na mechi zilizoko mbele yao.

Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu toka Mahakama Sports Klabu wakifanya dua ya pamoja kabla ya kuanza kwa mashindano na timu ya Wakala wa Uhifadhi wa Chakula mashindano yaliyofanyika katika viwanja vya shule ya sekondari Morogoro.
Wachezaji wa timu ya mpira wa miguu toka Mahakama Sports Klabu wakionesha ishara ya idadi ya mabao watakayoifunga timu ya NFRA kabla ya mpira kuanza.

  Baadhi ya wanamichezo mbalimbali wanaounda Timu za Mahakama Sports Klabu wakiondoka katika viwanja vya shule ya sekondari Morogoro huku wakishangilia ushindi baada ya kuifunga timu ya NFRA.

   Kikosi cha kwanza toka timu ya mpira wa Miguu ya Mahakama Sports Klabu kilichocheza mechi thidi ya NFRA.

    Wachezaji wa NFRA (wenye jezi za kijani) wakisalimiana na wachezaji wa timu ya Mpira wa miguu kutoka Mahakama Sports Klabu kabla ya kuanza kwa mashindano.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni