TANZIA
Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha Mtumishi wake aliyekuwa Msaidizi wa Kumbukumbu Daraja la kwanza (I), Bw. Castory Philipo Komba kilichotokea jana tarehe 03 Aprili, 2023 katika Hospitali ya Mloganzila mkoani Pwani alipokuwa akipatiwa matibabu.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 04 Aprili, 2023 na Mkurugenzi wa Usimamizi wa Kumbukumbu na Nyaraka, Mahakama ya Tanzania, Bw. Malimo Manyambula msiba upo nyumbani kwa marehemu Goba-Kontena jijini Dar es Salaam na mazishi yanategemewa kufanyika kesho Jumatano tarehe 05 Aprili, 2023 katika makaburi ya Kondo Ununio jijini humo.
Ratiba ya mazishi itatolewa mara baada ya familia yake kuikamilisha.
Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki kuomboleza katika kipindi hiki kigumu cha kuondokewa na mpendwa wetu.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni