Na William Mogore-Divisheni ya Makosa ya Rushwa
Watumishi wa Mahakama Kuu
ya Tanzania, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu
Uchumi wamepigwa msasa kwenye Mfumo wa Kuratibu Mashauri ulioboreshwa
unaojulikana kama Advanced Case Management System (e-CMS).
Mafunzo hayo yaliendeshwa
jana tarehe 13 Aprili, 2023 na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni hiyo Mhe. Magdalena
Ntandu akishirikiana na Afisa Teknolojia wa Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Bw. William
Mogore.
Mhe. Naibu Msajili
alisema, "Mfumo wa Mashauri umeboreshwa sana na zile changamoto tulizokuwa
tunakumbana nazo kwa kiasi kikubwa zimetatuliwa. Lakini pia Mfumo mpya umeunganishwa
na wadau wetu ambao ni Ofisi ya Mashtaka, NIDA, BRELA na wengine."
Alisema mfumo huo unawaweka
karibu na wadau waMahakama. Aliendelea kusema, "Mfumo pia unafanya kazi ya
kupangia mashauri moja kwa moja (Automatic Assignment). Kadhalika, mfumo
unaruhusu kubadili upangiaji huo kwa kuchagua Jaji, Naibu Msajili au Hakimu
Mfawidhi kwa njia ya kawaida."
Aliwashukuru watumishi
wote walioshiriki kwenye mafunzo hayo na kuwaasa waupokee mfumo huo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni