Na Arapha Rusheke, Mahakama-Dodoma.
Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dodoma imetoa mafunzo kwa watumishi pamoja na wadau wa Mahakama juu ya utumiaji wa mfumo mpya wa usimamizi wa mashauri (e-Case Management System) ili kuwawezesha kuendelea kuongeza ufanisi katika kazi.
Akifungua mafunzo hayo na siku tatu yaliyofanyika hivi karibuni katika Ukumbi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Dodoma (IJC) Kaimu Jaji Mfawidhi Kanda ya Dodoma Mhe. Dkt Fatma Rashid Khalfan amewaasa watumiaji wa mfumo huo kuzingatia taratibu na sheria.
“Mnatakiwa kutumia elimu mliyonayo,ujuzi mtakaoupata katika mafunzo haya ili kuboresha na kutatua changamoto ambazo zitajitokeza katika mfumo huu,” alisema. Dkt Fatma.
Aliongeza kuwa kundi la kwanza kupata mafunzo hayo litakuwa kundi la Mahakimu wote wa Kanda ya Dodoma kwa ngazi ya Mahakama za Hakimu Mkazi zote na Mahakama za Wilaya zote pamoja na watumishi wengine. wa Mahakama. Kundi la pili litahusisha wadau wote wanaoshughulika na Mahakama kama, Ofisi ya Mashtaka, Ofisi ya Mpelelezi wa Makosa ya Jinai ngazi ya Mkoa (RCO), Ustawi wa Jamii, Uhamiaji,Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi ngazi ya Mkoa (OCCID) .
Ofisi zingine ni Magereza na Ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Kundi la tatu litahusisha Ofisi ya Wakili Mkuu wa Serikali na Mawakili wa Kujitegemea (TLS).
Naye Naibu Msajili wa Kanda ya Dodoma, Mhe.Silvia Lushasi alisema kuwa lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uelewa juu ya kutumia njia za kiielektroniki (Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)ili kurahisisha uendeshaji wa shughuli za mbalimbali za Mahakama na hatimaye kufikia lengo la uborehaji wa huduma ya utoaji haki kwa wananchi.
Akitoa mada kuhusu mfumo huo, Afisa TEHAMA wa Kanda ya Dodoma, Bw.Ally Daudi alisema dhima ya mfumo huo ni kurahisisha kazi lakini pia kuwezesha utendaji kazi wa Mahakama kuwa rahisi na wenye ubora, usalama na Madhubuti kwa mtumiaji na watumiaji. Hivyo washiriki wote wa mafunzo hayo waliaswa kuongeza kasi katika matumizi ya mifumo ya TEHAMA ili kuokoa muda na gharama za huduma.
Kaimu Jaji Mfawidhi Kanda ya Dodoma, Dkt .Fatma Rashid Khalfan (mwenye kilemba) akisema neno la ufunguzi wakati wa mafunzo mfumo mpya wa usimamizi wa mashauri (e-case management) katika ukumbi wa Mahakama uliopo Kituo Jumuishi (JIC) jijini Dodoma.
Mahakimu wa Kanda ya Dodoma, wakifuatilia mada ya mfumo huo mpya.
Wadau wa mahakama wakiwa katika picha ya Pamela na Naibu Msajili Kanda ya Dodoma na Singida Mhe. Silivia Lushasi (aliyekaa katikati).
Washiriki na wadau wa mahakama wakiwa katika picha ya pamoja na Naibu Msajili Kanda ya Dodoma, Mhe. Silivia Lushasi (aliekaa katikati).
Afisa TEHAMA wa Kanda ya Dodoma,
Bw.Ally Daudi akitoa mada katika mafunzo hayo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni