Alhamisi, 20 Aprili 2023

WATUMISHI WA MKOA LINDI WANOLEWA MFUMO MPYA WA USIMAMIZI MASHAURI

Na Hillary Lorry. Mahakama,Lindi


Kaimu Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi Bw. Faustine  Allo amewaasa washiriki wote mafunzo ya mfumo mpya wa Usimamizi wa Mashauri  ujulikanao kwa jina la (Advanced e - Case Management System)  katika mkoa wa Lindi kuulewa mfumo huo kwa kuwa unasadia kuboresha utendaji wao wa kazi.


Akizungumza wakati akizungumza tarehe 19 Aprili, 2023 wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika  Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi, alisema  yanahutaji  uelewa wa pamoja ili kuendelea kutimiza jukumu la utoaji haki kwa wote na wakati.


Kwa upande wake, Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya ya Lindi Mhe. Maria Batulaine aliwataka washiriki hao kuwa tayari kumsikiliza kwa makini mtoa mada juu ya mfumo huo, ambaye ni Afisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) Kanda ya Mtwara, Bw. Richard Matasha ili waweze kuelewa vizuri matumizi  yake kwa usahihi.


Mfumo ambao ni mbadala wa mfumo wa awali wa Upokeaji na Uratibu wa ashauri (JSDS II), hivyo watumishi waliopata fursa hiyo ni Wasaidizi wa Kumbukumbu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi, na Wasaidizi wa Kumbukumbu na Mahakimu wa wilaya zote tano zilinazopatikana katika Mkoa wa Lindi.


Naye Mwezeshaji wa mafunzo hayo Afisa TEHAMA, Matasha  kabla ya kuanza kufundisha alielezea kwa ufupi faida za mfumo huo mpya ukilinganisha na mfumo wa awali JSDS II ambapo alisema kuwa mfumo wa mpya wa upokeaji na uratibu wa mashauri  umeboreshwa kuanzia shauri linapofunguliwa mpaka shauri linapofikia tamati (Judgment).

Aliongeza kuwa mfumo huo ni shirikishi kwani haujaishia mahakamani tu bali hata wadau wamehusishwa, Ni muhimu kuchukua hatua za makusudi na kujimilikisha  ili kupata matokeo chanya na yenye manufaa,” alisisitiza Matasha.


Wakati huohuo, Mhe. Maria aliwapongeza Mahakimu wote  na Wasaidizi wa Kumbukumbu (makarani) kwa kazi nzuri waliyoifanya  katika mfumo wa JSDS II kwani walihakikisha mashauri yote yanaingizwa na kuhuishwa kwa wakati jambo lililoleta urahisi wa upatikanaji wa taarifa sahihi kwa wakati.


Hakimu Mkazi Mfawidhi Wilaya ya Lindi, Mhe. Maria Batulaine akizungumza jambo na watumishi wa Mahakama Mkoa wa Lindi(hawapo kwenye picha)


Hakimu Mkazi Mfawaidhi Wilaya ya Ruangwa,Mhe. Mariam Mchomba akielrezea jambo.


Mwezeshaji wa mafunzo hayo, ambaye pia ni Afisa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano(TEHAMA) alita mada.

Watumishi wa Mahakama Mkoa wa Lindi wakimsikiliza mwezeshaji.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni