Na. Innocent Kansha-Mahakama
Chuo
cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) kimeingia makubaliano ya ushirikiano na
Chuo cha Diplomasia “Centre for Foreign Relation” wenye lengo kuwajengea uwezo
uwezo watumishi wa Mahakama kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la itifaki na
adabu “Protocal and Etiquette”
Makubaliano
hayo yamesainiwa leo tarehe 22 Mei, 2023 Mahakama ya Rufani ya Tanzania jijini
Dar es salaam kati ya Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) na
Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Mhe. Dkt. Paul Faustin Kihwelo pamoja
na Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia Kurasini, Bw. Felix Wandwe.
“Makubaliano
hayo yanalenga kujengeana uwezo katika nyanja mbalimbali ikiwemo utafiti,
ushauri wa kitaalamu na uandaaji wa mafunzo, mikutano, warsha na makongamano”,
alisema Jaji Dkt. Kihwelo
Jaji
Dkt. Kihwelo aliongeza kuwa makubalianao hayo yamefanyika wakati muafaka ili
kukuza uelewa na weledi wa namna bora ya kuratibu na shughuli/hafla mbalimbali
za kimahakama na Chuo.
“Mfano
katika Taasisi kama Mahakama, Maafisa wengi hupendelea kuvalia tai yenye rangi
nyekundu lakini ukifuata misingi ya itifaki na adabu tai nyekundu inapaswa
kuvaliwa na Mkuu wa Mhimili yaani Jaji Mkuu wa Tanzania, jambo hili limekuwa
likitolewa elimu mara kwa mara kuepusha kuharibu itifaki” alisema Jaji Dkt.
Kihwelo.
Jaji
Dkt. Kihwelo aliongeza kuwa tayari Chuo kimeandaa andiko maalumu la kuratibu
shughuli zote zinazohusu itifaki na adabu na litawasilishwa Chuo cha Diplomasi
ili kushirikishana kwa lengo la kuboresha zaidi.
Kwa
upande wake, Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia Bw. Felix Wandwe hakusita kutoa
shukrani zake kwa kusaini makubaliano na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto
(IJA) katika mashirikiano ya kuboresha ujuzi katika eneo la itifaki na adabu.
“Binafsi
nimekitembelea Chuo cha IJA na nimeona kuna mambo mengi sana tuayoweza kufanya
kazi pamoja kama vile masuala ya upatanishi na usuluhishi, mbinu za majadiliano
(negotiations skills) tuna Walimu wabobevu pale Chuo cha Diplomasia na hasa
ndiyo maeneo tuliojikita kutoa elimu zaidi ya masuala ya itifaki na adabu”,
alisema Mkurugezi huyo.
Bw.
Wandwe aliongeza kuwa, kuna mambo mengi yanayofanywa na Chuo cha Diplomasia
yanayoingiliana moja kwa moja na shughuli za kimahakama za utatuzi wa migogoro,
ushauri kwa viongozi na kuwaongezea weledi katika mbinu za kutatua migogoro.
Bw.
Wandwe alisema, katika utekelezaji wa makubaliano hayo utaandaliwa Mpango Kazi
utakaosaidia kutekeleza majukumu yaliyoainisha ndani ya makubaliano hayo, kwa
maana ya kuonyesha muda maalumu wa utekelezaji wa kila shughuli iliyoanishwa.
“Uzoefu
unaonyesha kuwa makubaliano mengi yanayoingiwa kati ya taasisi nyingi yamekuwa
hayatekelezi kwa sababu ya kutokuwa na muda maalumu wa utekelezaji wa majukumu
yaliyoanishwa kufanyiwa kazi, hili letu litafanyika kwa nguvu zote
kulifanikisha”, aliongeza Mkurugenzi huyo.
Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) na Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Mhe. Dkt. Paul Faustin Kihwelo (kushoto) pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia Kurasini, Bw. Felix Wandwe (kulia) wakikabidhiana hati za mashirikiano mara baada ya kutia saini makubaliano ya ushirikiano wenye lengo kuwajengea uwezo watumishi wa Mahakama kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la itifaki na adabu “Protocal and Etiquette” leo tarehe 22 Mei, 2023 Mahakama ya Rufani, jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA) na Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Mhe. Dkt. Paul Faustin Kihwelo (kushoto) pamoja na Kaimu Mkurugenzi wa Chuo cha Diplomasia Kurasini, Bw. Felix Wandwe (kulia) wakitia saini makubaliano ya ushirikiano wenye lengo kuwajengea uwezo watumishi wa Mahakama kwenye maeneo mbalimbali ikiwemo eneo la itifaki na adabu “Protocal and Etiquette”
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni