Jumatano, 3 Mei 2023

JAJI KIONGOZI KUONGOZA ZOEZI LA KUWAAGA KITAALUMA MAJAJI WATATU WASTAAFU WA MAHAKAMA KUU

Na Tiganya Vincent- Mahakama

Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika sherehe ya kuwaaga kitaaluma Majaji watatu wa Mahakama Kuu ambao wamestaafu kwa mujibu wa sheria.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msajili Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sharmillah Sarwatt Majaji Wastaafu hao wataagwa kitaaluma tarehe 04 Mei, 2023 katika ukumbi namba moja (1) wa Mahakama Kuu ya Tanzania Jijini Dar es Salaam.

Majaji ambao wanatarajiwa kuagwa Kitaaluma ni pamoja na Mhe. Sekela Cyril Moshi,  Mhe. Beatrice Rodah Mutungi na Mhe. John Samwel Mgetta.

Zoezi hilo linafanyika kwa mujibu wa Waraka Na. 1 wa Mwaka 2006 wa Jaji Mkuu.


Jaji Kiongozi -Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni