Ijumaa, 19 Mei 2023

JAJI MKUU AAHIRISHA KIKAO CHA BARAZA LA WAFANYAKAZI WA MAHAKAMA

Na Arapha Rusheke, Mahakama Kuu Dodoma

Jaji Mkuu wa Tanzania na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi wa Mahakama nchini, Mhe.Prof.Ibrahim Hamis Juma ameahirisha kikao cha siku mbili cha Baraza Kuu la wafanyakazi wa Mhimili huo kilichokuwa kikifanyika katika Ukumbi wa PSSSF jijini Dodoma.

Akihairisha kikao hicho leo tarehe 19 Mei, 2023, Jaji Mkuu ameahidi hoja zote zitafanyiwa kazi na kufuatiliwa na kuhakikisha kwamba yanafanyiwa kazi kwani lengo ni kuboresha mazingira ya utoaji huduma sambamba na kuboresha maslahi watumishi kwa ngazi zote za Mahakama. 

“Mkutano wetu wa siku mbili umekuwa na masomo mengi sana. Mimi naamini kila mmoja wetu amejifunza kitu kwa sababu tumekuja kwa nia ya kusikilizana, kujifunza changamoto mbalimbali kutoka sehemu mbalimbali na kuna mambo mengi sana ambayo tumejifunza. Mimi binafsi naweza kusema nimejifunza mengi sana,’’ amesema Jaji Mkuu.

Miongoni mwa maazimio yaliyofikiwa katika kikao hicho ni pamoja na Watumishi wa Mahakama wapatiwe wapatiwe mafunzo ya msingi (basic knowledge) ya TEHAMA na matumizi ya mifumo ya KITEHAMA iliyopo mahakamani katika utoaji haki kwa kutumia mtaala ulioandaliwa ili wasaidie Mahakama ya Tanzania kuwa sehemu ya dunia ya kidijitali na uchumi wa maarifa.

Azimio lingine ni watumishi wanaokaribia kustaafu wapatiwe mafunzo kila robo mwaka na taarifa ya utekelezaji wake isambazwe kwenye Kanda zote.

Lingine ni ripoti ya utafiti uliofanywa na REPOA kuhusu kuridhika kwa watumiaji wa huduma za mahakama (court user satisfaction survey) ya mwaka 2023 itakapochapishwa, itafsiriwe kwa Kiswahili na isambazwe kwa watumishi wote ili waisome na kujipima utendaji wao.


Jaji Mkuu wa Tanzania na Mwenyekiti wa Baraza la Wafanyakazi Mahakama ya Tanzania, Mhe.Prof.Ibrahim Hamis Juma, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akizungumza jambo alipokuwa akiahirisha kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania leo tarehe 19 Mei, 2023 katika ukumbi wa PSSSF jijini Dodoma. Kushoto ni Katibu wa Baraza la Wafanyakazi, Mahakama ya Tanzania, Bw. Ezra Kyando na kulia ni Katibu Msaidizi wa Baraza la Wafanyakazi Mahakama ya Tanzania, Bi. Christina Mlwilo.
Jaji wa Mahakama ya Rufani na Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi Mahakama ya Tanzania, Mhe. Augustine Mwarija pamoja na sehemu ya Wajumbe wa Kikao hicho wakifuatilia kwa makini kinachojiri.

Jaji Kiongozi Mahakama Kuu ya Tanzania ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani (katikati), Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Masjala Kuu na Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi Mahakama ya Tanzania, Mhe. Moses Mzuna (kulia), Msajili Mahakama Kuu ya Tanzania na Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi la Mahakama ya Tanzania, Mhe. Sharmillah Sarwatt (kushoto) na sehemu ya Wajumbe wa Baraza hilo wakimsikiliza Mwenyekiti wa Baraza hilo, Mhe. Prof. Juma (hayupo katika picha) wakati akiahirisha kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania. 

Wajumbe wa Baraza la Mahakama ya Tanzania wakiwa katika Kikao cha Baraza hilo.


Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Iringa ambaye pia ni Mjumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Ilvin Mugeta akisoma maazimio ya Kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni