Ijumaa, 19 Mei 2023

MAANDALIZI UJENZI WA VITUO JUMUISHI VYA UTOAJI HAKI TISA YASHIKA KASI

Na Tiganya Vincent, Mahakama-Dodoma

Mahakama ya Tanzania imeanza kufanya maandalizi ya awamu ya pili ya ujenzi wa Vituo Jumuishi vya Utoaji Haki (IJCs) tisa (9) yanayotarajiwa kujengwa katika maeneo ambayo hayana huduma za Mahakama Kuu nchini.

Akiwasilisha Mada katika kikao cha Baraza Kuu la Wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania kinachofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa PSSSF jijini Dodoma, Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel alisema tayari michoro ya majengo hayo imekamilika huku taratibu nyingine zikiendelea.

“Mahakama imepanga kujenga Vituo Jumuishi vya Utoaji Haki (IJCs) tisa, vituo hivyo vinatarajiwa kujengwa kaatika Mikoa ya Singida, Simiyu, Geita, Songwe, Katavi, Njombe, Pwani, Lindi na Pemba,” amesema Mtendaji Mkuu.

Sanjari na hilo, Prof. Ole Gabriel alisema Mahakama inatarajia pia kuanza ujenzi wa Mahakama za Mwanzo 60 katika maeneo mbalimbali hapa nchini ambapo alizitaja Mahakama hizo ambazo ni pamoja na Kariakoo, Magomeni, Mbagala, Kimanzi Chana, Bunju, Mipingo, Pande, Ndonomi, Chikongola, Chikindu.

Nyingine ni Kitangali, Kasanga, Namanyere, Nambogo, Ugala, Sibwesa, Mamba, Lupatingatinga, Ndobo, Rujewa, Kanga, Msangano, Inchwankima, Kasamwa, Izigo, Katoro, Kigoma Kaskazini, Herujuu na Manyovu.

Maeneo mengine ambapo zitajengwa Mahakama hizo ni Minnyunge, Unyamkumbi, Kwamtoro, Minjingu, Terrat, Engasment, Maji ya chai, Makuyuni, Muriet, Sanya Juu, Tarakea, Gonja, 12 Sengerema Urban, Nyanguge, Misasi, Mugumu, Lagangabilili, Mhango, Somanda, Shinyanga, Kahama, Bwakila Chini, Minepe, Mafinga, Izazi, Masasi, Lupembe, Likuyusekamaganja, lilondo na Nalasi.

Aidha , Mtendaji Mkuu huyo wa Mahakama alisema , Mahakama inaendelea na ujenzi na ukarabati wa Majengo ya Mahakama za Wilaya tano (5) za Ubungo, Ulanga (Mahenge), Liwale, Kwimba na Korogwe, pamoja na ukarabati wa jengo la Mahakama ya wilaya Maswa.

Aliongeza kuwa Mahakama iko katika hatua za mwanzo za kuanza ujenzi wa Mahakama za Wilaya kumi na tano (15) ambazo ni Mahakama za Wilaya za Kalambo, Nachingwea, Kibiti, Mbulu, Masasi, Tarime, Mkalama, Tunduru, Nkasi, Simanjiro, Nyasa, Ukerewe, Chamwino, Kilosa na Momba.

Prof. Ole Gabriel aliongeza kuwa ujenzi wa Mahakama za Mwanzo tisa (9) unaendelea katika katika maeneo ya Kinesi (Rorya), Kabanga (Ngara), Madale (Kinondoni), Mahenge (Kilolo), Mlimba, Mang'ula (Morogoro), Luilo (Ludewa), Usevya (Mlele) na Newala (Mtwara).

Wakati huohuo, Mtendaji mkuu alisema kwamba, Mahakama ipo katika hatua za mwanzo za kuanza Ujenzi wa Mahakama nyingine za Mwanzo 12 ambazo ni Maore, Mwimbi, Rungwa, Nanjilinji, Kipili, Ilangala, Machame, Ketumbeine, Haubi, Kinusi, Magubike na Mbalizi.


Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel akitoa taarifa katika Mkutano wa Baraza la Wanyakazi wa Mahakama jana tarehe 18 katika ukumbi wa PSSF jijini Dodoma.

Baadhi ya Wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi wa Mahakama ya Tanzania wakifuatilia taarifa ya Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel (hayupo katika picha) wakati akiwasilisha mada katika kikao cha siku mbili kilioanza jana tarehe 18 Mei 2023.






 


 



Hakuna maoni:

Chapisha Maoni