Jumatatu, 29 Mei 2023

MAHAKAMA YA TANZANIA, CHUO KIKUU CAPE TOWN KUSHIRIKIANA KUBORESHA MFUMO WA KUTUNZA MAAMUZI

Na. Innocent Kansha-Mahakama

Mahakama ya Tanzania imeingia makubaliano ya ushirikiano na Chuo Kikuu cha Cape Town Afrika ya Kusini wenye lengo kuendeleza juhudi za kuboresha mfumo maalumu wa kutunza maamuzi ya kimahakama TanzLII na kutengeneza namna bora ya ufikiaji na upatikanaji bure wa Maamuzi, Sheria na Kanuni za Tanzania kwa njia ya Mtandao “TanzLII - Access Court Decisions and Laws of Tanzania for Free”.

Makubaliano hayo yamesainiwa leo tarehe 29 Mei, 2023 Mahakama Kuu Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Temeke jijini Dar es salaam kati ya Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Wilbert Martin Chuma kwa upande wa Mahakama ya Tanzania pamoja na Mkurugenzi wa AfricanLII Bi. Mariya Badeva. Huku utiwaji saini huo ukishudiwa na  Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania na Kamishina wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Mhe. Dkt. Gerald Ndika.

Tukio hilo lilienda sambamba uzinduzi wa Tovuti ya TanzLII iliyofanyiwa uboreshaji mkubwa na Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania na Kamishina wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Mhe. Dkt. Gerald Ndika.

Habari picha na matukio mbalimbali yaliyojili katika shughuli hiyo.

Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Wilbert Martin Chuma (kulia)kwa upande wa Mahakama ya Tanzania akitia saini makubaliano ya ushirikiano ya kuimarisha mfumo wa kutunza maamuzi ya kimahakama pamoja na Mkurugenzi wa AfricanLII Bi. Mariya Badeva (kushoto). Huku utiwaji saini huo ukishudiwa na  Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania na Kamishina wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Mhe. Dkt. Gerald Ndika, leo tarehe 29 Mei, 2029 katika hafla iliyofanyika Mahakama Kuu Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Temeke jijini Dar es salaam. 

Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania na Kamishina wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Mhe. Dkt. Gerald Ndika, leo tarehe 29 Mei, 2029 amezindua toleo la tatu la tovuti mpya ya mfumo wa kutunza maamuzi ya kimahakama wenye lengo la kuboresha ufikiaji na upatikanaji bure wa Maamuzi, Sheria na Kanuni za Tanzania kwa njia ya Mtandao “TanzLII - Access Court Decisions and Laws of Tanzania for Free”,  katika hafla iliyofanyika Mahakama Kuu Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Temeke jijini Dar es salaam. 

Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Wilbert Martin Chuma (kulia) akibalisha hati za makubaliano mara baada ya kutia saini na Mkurugenzi wa AfricanLII Bi. Mariya Badeva (kushoto) kutoka Chuo Kikuu cha Cape Town Afrika ya kusini, nyuma yao ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania na Kamishina wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Mhe. Dkt. Gerald Ndika aliyeshuhudia utiaji wa saini makubaliano hayo.

Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Wilbert Martin Chuma (kulia) na Mkurugenzi wa AfricanLII Bi. Mariya Badeva (kushoto) kutoka Chuo Kikuu cha Cape Town Afrika ya kusini, akionyesha hati zililzosainiwa za kukubali mashirikiano hayo.

Majaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania na wa Mahakama Kuu (walioketi mstari wa mbele) waliohudhuria hafla ya uzinduzi wa tovuti ya kutunza maamuzi TanzLII toleo la Tatu sambamba na utiaji saini makubaliano ya ushirikiano wa lengo la kuboresha ufikiaji na upatikanaji bure wa Maamuzi, Sheria na Kanuni za Tanzania kwa njia ya Mtandao “TanzLII - Access Court Decisions and Laws of Tanzania for Free”, wakimsikiliza Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Manyara Mhe. John Kahyoza (hayupo pichani) akitoa historia fupi ya mchakato wa uanzishwaji wa mfumo wa kutunza maamuzi TanzLII wakati wa hafla hiyo.Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania na Kamishina wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Mhe. Dkt. Gerald Ndika (wa nne kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya Majaji walishiriki hafla hiyo, wengine ni Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Mhe. Jacobs Mwambegele (wa pili kushoto), Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma Mhe. Dkt. Adam Mambi (wa tatu kulia), Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Manyara Mhe. John Kahyoza (wa kwanza kulia), Kaimu Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu Temeke (IJC) Mhe. Asina Omari (wa pili kulia), Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Iringa Mhe. Said Kalunde (wa kwanza skushoto) pamoja na Mkurugenzi wa AfricanLII Bi. Mariya Badeva (wa nne kushoto) akiwa na Meneja Mradi wa sheria Africa Bi. Morina Chindia (wa tatu kushoto).
 

Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania na Kamishina wa Tume ya Utumishi wa Mahakama Mhe. Dkt. Gerald Ndika (wa sita kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya machampioni wa mfumo wa kutunza maamuzi ya kimahaka TanzLII wengine katika picho hiyo ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Wilbert Martin Chuma (wa tano kulia) na Mkurugenzi wa AfricanLII Bi. Mariya Badeva (wa saba kushoto)   walishiriki hafla hiyo.


 Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Manyara na Championi wa mfumo wa TanzLII Mhe. John Kahyoza (wa kwanza kulia) akitoa historia fupi ya mfumo huo wakati wa uzinduzi wa toleo la Tatu la mfumo huo, kushoto ni Kaimu Mkuu wa huduma za Maktaba ya Tanzania, Mhe. Kifungu Mrisho.


Mkurugenzi wa AfricanLII Bi. Mariya Badeva ( kushoto) akiwa na Meneja Mradi wa sheria Africa Bi. Morina Chindia (Kulia) wakifuatilia shughuli hiyo.

(Picha na Innocent Kansha-Mahakama)
 Hakuna maoni:

Chapisha Maoni