Na Eva Leshange- Mahakama, Singida
Jaji Mfawidhi Mahakama
Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Gerson Mdemu hivi karibuni alioongoza
kikao cha awali kwa ajili ya maandalizi ya vikao maalumu vya kusikiliza
mashauri ya jinai (criminal session) vitakavyofanyika mkoani hapa.
Taarifa ya ufunguzi
iliyosomwa na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Dodoma, Mhe. Silivia
Lushasi inaeleza kuwa jumla ya mashauri 17 ya jinai yanategemewa kushughulikiwa
ndani ya mwezi mmoja. Vikao hivyo vimeanza tangu tarehe 15 Mei, 2023 na vinategemewa
kumalizika tarehe 14 Juni, 2023.
“Sambamba na taarifa hii,
Mkoa wa Singida una mashauri 30 ambayo yanasubiri kusikilizwa ambapo katika Mahakama
ya Hakimu Mkazi Singida kuna mashauri 18, Iramba nane na Manyoni manne,” alisema.
Mhe. Lushasi alibainisha
kuwa mashauri tajwa hayahusishi mashauri yanayosubiri washitakiwa kusomewa mashtaka
yao kwa mara ya kwanza (plea taking). Aliwasisitiza pia wadau, wakiwemo Ofisi
ya Mwendesha Mashtaka, Mawakili wa Kujitegemea na Jeshi la Magereza kuhakikisha kesi zilizopanga
zinafanikiwa kwa aslilimia 100.
Naibu Msajili alieleza
kuwa kuandaa vikao hivyo ni gharama, hivyo ni jambo zuri kama thamani ya fedha
(value for money) itaonekana na kuzaa matunda.
Kwa upande wao, wadau hao wa haki jinai waliahidi kushirikiana na Mahakama ili kufanikisha lengo lililokusudiwa la kusikiliza na kumaliza mashauri yote ambayo yamepangwa kushughulikiwa katika kikao hicho maalumu.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania,
Kanda ya Dodoma, Mhe. Gerson Mdemu (katikati) akifaanua jambo katika
kikao hicho.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya
Dodoma, Mhe. Silivia Lushasi akisoma taarifa fupi ya mashauri.
Sehemu ya wajumbe wa haki jinai waliohudhuria
kikao hicho.
Wakili wa Kijitegemea Hemed Kulungu
akichangi ajambo.
Wakili wa Serikali Almachus Bagenda
akichangia jambo katika kikao hicho.
(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni