Na Hillary Herman
Naibu Msajili Mahakama
Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mtwara, Mhe. Lukuna Fredrick jana tarehe 15 Mei, 2023
alifanya ziara katika Mahakama ya Wilaya Nachingwea kukagua shughuli mbalimbali
za kimahakama.
Katika ziara hiyo, Mhe.
Fredrick aliongoza kikao cha watumishi wa Mahakama hiyo na kujadili mambo
mbalimbali ya kiutendaji na utumishi.
Kikao hicho kilichofanyika
katika ukumbi wa Mahakama hiyo kilihudhuriwa pia na viongozi waandamizi wa
Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mtwara, akiwemo, Mtendaji, Bw. Richard
Mbambe pamoja na Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi, Mhe.
Consolata Singano.
Baada ya kufungua kikao
hicho, Mhe. Lukuna alipokea taarifa ya
utekelezaji wa majukumu kutoka kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya
ya Nachingwea, Mhe. Sikitu Mwalusamba.
Akizungumza na watumishi
katika kikao hicho, Naibu Msajili alisisitiza kutunza mali za Mahakama kwa
uangalifu mkubwa ili ziweze kudumu kwa muda mrefu na kutumika na vizazi
vijavyo.
“Mali hizi tunazozitumia
zipo hadi leo kwa sababu zilitunzwa na waliotangulia, tuzitumie kwa uangalifu
mkubwa, tuzitunze na kuzilinda kusudi zidumu na vizazi vingine viweze kuzikuta,”
alisema.
Kadhalika, Mhe. Lukuna
alisisitiza watumishi kutoa huduma nzuri kwa wateja, kufanya kazi kwa bidii na
kushirikiana na wadau wa Mahakama.
Pia alisisitiza kutekeleza Mpango Mkakati wa Mahakama wa miaka mitano (2020/2021 – 2024/2025) na kuwasihi kujiendeleza kielimu katika taaluma zao pamoja na matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ili kwenda na kasi ya mabadiliko ya Mahakama.
Naibu Msajili Mahakama Kuu
ya Tanzania, Kanda ya Mtwara, Mhe. Lukuna Fredrick (katikati) akiwasili katika
viunga vya Mahakama ya Wilaya ya Nachingwea.
Naibu Msajili Mahakama Kuu
ya Tanzania, Kanda ya Mtwara, Mhe. Lukuna Fredrick akisaini kitabu cha wageni.
Hakimu Mkazi Mfawidhi
Mahakama ya Wilaya Nachingwea, Mhe. Sikitu William Mwalusamba (aliyesemama)
akimkaribisha na kumtambulisha Naibu Msajili na jopo aliloongozana nalo.
Naibu Msajili Mahakama Kuu
ya Tanzania, Kanda ya Mtwara, Mhe. Lukuna Fredrick (aliyesimama) akiongea na
watumishi (hawapo kwenye picha).
Mtendaji wa Mahakama Kuu,
Kanda ya Mtwara, Bw.Richard Mbambe (aliyesimama) akiongea na watumishi.
Hakimu Mkazi Mfawidhi
Mahakama ya Hakimu Mkazi Lindi, Mhe. Consolata Singano akielekeza jambo.
Mtumishi akichangia katika mada zilizowasilishwa.
(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni