Jumatano, 10 Mei 2023

TANZIA; MTUMISHI MAHAKAMA KUU SHINYANGA AFARIKI DUNIA



Marehemu Christina Kabula Sotery enzi za uhai wake.

TANZIA

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Mtumishi wake Bi. Christina Kabula Sotery aliyekuwa akihudumu Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Shinyanga kama Msaidizi wa Ofisi Mkuu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 10 Mei, 2023 na Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Shinyanga, Bi. Mavis Miti marehemu Christina amefariki usiku wa kuamkia leo katika Hospitali ya Rufaa Shinyanga alipokuwa akipatiwa matibabu baada ya kuanguka ghafla jana tarehe 9 Mei, 2023 akiwa Ofisini akitekeleza majukumu yake. 

Bi. Mavis amesema mipango ya mazishi inafanywa na mazishi yanatarajiwa kufanyika Ijumaa tarehe 12 Mei, 2023 mkoani Shinyanga.

Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki kuomboleza msiba huu wa kuondokewa na Mpendwa wetu.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.






 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni