Na Amina Said-Mahakama, Temeke
Uongozi wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia
Temeke umewatunuku vyeti watumishi waliofanya vizuri mwaka 2022 katika kutimiza
majukumu yao ya kila siku, kama njia moja wapo ya motisha na kutambua kazi wanazozifanya.
Hafla hiyo fupi imefanyika leo tarehe 5 Mei, 2023 katika
ukumbi wa Mikutano wa Kituo hicho, ambapo jumla ya Mahakimu 12 wa Mahakama ya
Mwanzo wamepongezwa kwa kuhakikisha hakuna mashauri ya mrundikano.
Wakati huo huo, Afisa Teknolojia Habari na Mawasiliano
(TEHAMA), Bi. Amina Said amepongezwa kwa jitihada zake za kubuni na kujenga mifumo
ya TEHAMA. Kadhalika, Msaidizi wa Kumbukumbu, Bw. Zuberi Bakari, nae
alitunukiwa cheti kwa kuchaguliwa kuwa mfanyakazi bora wa mwaka 2023.
Akizungumza katika hafla hiyo, Jaji Mfawidhi wa Kituo hicho,
Mhe. Zainabu Goronya amewaomba watumishi wote kuendelea kufanya kazi kwa bidi.
Amesema anatambua upungufu wa watumishi uliopo, hivyo kuahidi
kuwasiliana na uongozi wa Mahakama ya Tanzania kuangalia uwezekano wa kuongeza idadi
ya Mahakimu. hasa katika Mahakama ya
Wilaya ili kupunguza mzigo wa mashauri waliyonayo katika Mahakama hiyo.
Jaji Mfawidhi wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke, Mhe. Zainabu Goronya akikata keki. Kulia ni Naibu Msajili wa Mahakama Kuu katika Kituo hicho, Mhe. Martha Mpaze.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni