Na Eva Leshange-Mahakama Singida
Chama
cha Majaji na Mahakimu (JMAT) Tawi la Singida hivi karibuni
kilikutana kujadili masuala mbalimbali ya kazi na kupeana mbinu za kuinuana kiuchumi.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa
Mahakama ya Mkoa wa Singida, Mhe. Allu Nzowa ndiye aliyefungua Kikao hicho
ambacho kilichofanyika katika Wilaya ya Manyoni.
Kufanyika kwa Kikao hicho
ni muendelezo wa vikao ambavyo wanachama wa JMAT wamekuwa wakifanya mara kwa
mara ili kujengeana uwezo na kujadili masuala ambayo Mahakimu hukutana nayo katika
vituo vyao vya kazi, kutatua changamoto na kupeana uzoefu na mbinu mbalimbali
za stadi za maisha.
Vikao hivyo vimekuwa na
tija hasa kwa Mahakimu wageni kwani wanapata fursa ya kujifunza mambo yanayohusu
tasnia kwa undani na kwa vitendo zaidi na pia vimekuwa msaada ambapo hukumbushana
sheria mbalimbali na mabadiliko yake.
Katika kikao hicho,
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Manyoni, Mhe. Alisile Mwankejela,
katika mada ya kupeana uzoefu aliwasisitiza Mahakimu kutojifungia ndani badala
yake wajishughulishe na shughuli nyinginezo za kujipatia kipato na
kutokutegemea mishahara pekee.
“Waheshimiwa wenzangu
tusijifungie ndani, tujiongeze kwa kufanya shughuli nyinginezo zitakazotuongezea
kipato ili kuboresha na kupunguza ukali wa maisha,” alisema.
Vile vile aliwapa uzoefu
alionao katika shughuli za ufugaji wa kuku, kilimo na biashara ya mazao na
mifugo.Wajumbe wengine walitoa uzoefu katika biashara mbalimbali.
Baada ya kupeana uzoefu wa kazi na mbinu za kuinuana kiuchumi ulifanyika uchaguzi wa Mwenyekiti wa JMAT Tawi la Singida baada ya Mwenyekiti aliyekuwepo awali kuhama Mkoa na Mhe. Esther Mpanga alishinda kwa kishindo.
Hakimu Mkazi
Mfawidhi wa Mahakama Hakimu Mkazi Singida, Mhe. Allu Nzowa akzungumza wakati
anafungua kikao kazi cha wanachama wa Chama cha Majaji na Mahakimu (JMAT) Tawi
la Singida.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama Hakimu Mkazi Singida, Mhe. Allu Nzowa (katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Mahakimu. Wengine waliokaa ni Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Manyoni, Mhe. Alisile Mwankejela(kushoto), Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Iramba, Mhe. Christopher Makwaya (wa pili kushoto), Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Manyoni Mjini, ambaye pia ni Katibu wa JMAT Tawil la Singida, Mhe. Gidion Kilaga na Mtendaji wa Mahakama Singida, Bw. Yusuph Kasuka.
Meza Kuu ikiongozwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama Hakimu Mkazi Singida, Mhe. Allu Nzowa (katikati waliokaa) ikiwa katika picha ya pamoja na
Mahakimu wa Mahakama ya Hakimu Mkazi na Wilaya Singida.
Meza Kuu ikiongozwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama Hakimu Mkazi Singida, Mhe. Allu Nzowa (katikati waliokaa) ikiwa katika picha ya pamoja na
Mahakimu wa Wilaya ya Manyoni.
Meza Kuu ikiongozwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama Hakimu Mkazi Singida, Mhe. Allu Nzowa (katikati waliokaa) ikiwa katika picha ya pamoja na Mahakimu wa Wilaya ya Iramba.
(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni