Na Mwinga Mpoli, Mahakama Kuu Mbeya
Watumishi wa Mahakama Mkoa wa Mbeya wamepatiwa mafunzo
ya afya ya akili ili kuboresha huduma wanazotoa kwa wateja kwa makundi yote.
Mafunzo hayo yalizinduliwa na Jaji Mfawidhi wa
Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya, Mhe. Dastan Ndunguru hivi karibuni
ambayo yalifanyika katika ukumbi wa Mahakama hiyo.
“Matatizo ya afya ya akili hayachagui, mtu yeyote
anaweza kuyapata. Sisi kama taasisi tunafaidika na mafunzo haya kwa sababu afya
ya akili ni kila kitu. Tukijiangalia hapa tunajiona tuna akili, lakini
tukipimwa tunaweza kujikuta wote tuna matatizo,” alieleza.
Kwa upande wake, Jaji wa Mahakama Kuu Mbeya ambae ni
mratibu wa mafunzo, Mhe. David Ngunyale alisema kuwa kutokuwa na utulivu wa
kiakili kunaweza kuathiri familia, mwajiri, wananchi na nafsi pia, hivyo ni
vema kuwa na mafunzo hayo ili kuweza kukabiliana na changamoto mbalimbali.
Jaji mwingine anayehudumu katika Mahakama hiyo, Mhe.
Victoria Nongwa, akizungumza wakati ana ahirisha mafunzo hayo alisisitiza watu
kujipenda na kupunguza matarijio makubwa.
(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni