Alhamisi, 1 Juni 2023

JAJI MAKUNGU ATEULIWA KUWA JAJI MAHAKAMA YA AFRIKA MASHARIKI

Na Mwandishi wetu

Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania, Mhe. Omar Othman Makungu ameteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Haki ya Afrika Mashariki, Divisheni ya Rufani.

Uteuzi huo ambao umefanyika mjini Bujumbura, Burundi katika Mkutano wa Marais wa Nchi Wanachama wa Afrika Mashariki Uliofanyika jana tarehe 31 Mei, 2023.

Mkutano huo ulifanyika kujadili mambo mbalimbali, ikiwemo suala la usalama Mashariki wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Majaji wengine walioteuliwa ni Mhe.Anita Mugeni kutoka Rwanda anayekuwa Makamu Rais wa Mahakama hiyo na Mhe. Kayembe Rene kutoka DRC ambaye anakuwa Jaji wa Mahakama katika Divisheni ya Awali.

Uteuzi wa Mhe. Makungu na Mhe. Mugeni utaanza rasmi tarehe 20 Juni, 2023, huku uteuzi wa Mhe. Kayembe umeanza jana tarehe 31, 2023.

Mhe. Makungu amewahi kuwa Jaji Mkuu wa Zanzibar kabla ya kuteliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ya Tanzania.


Mhe. Omar Othman Makungu.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni