Na Evelina Odemba – Mahakama Morogoro
Ukaguzi huo ulifanyika Mei 31, 2023 kwenye majengo hayo mapya na ya kisasa yaliyo katika hatua za umaliziaji ujenzi ambayo yapo Wilaya ya Kilombero na yamejengwa kwa fedha za mapato ya ndani ikiwa ni Mpango Mkakati wa Mahakama ya Tanzania wa kusogeza huduma za Mahakama karibu na wananchi.
Akiwa katika jengo la Mahakama ya Mwanzo Mlimba lililo umbali wa kilomita 380 toka Manispaa ya Morogoro Mhe. Ngwembe alimwagia sifa muonekano wa jengo hilo na kusema kuwa “jengo hili limekamilika kwa kiwango kikubwa na lina muonekano mzuri wa kisasa” alisema.
Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Mlimba, Mhe.Deodatus Kwembe alisema Mahakama hiyo inasikiliza takribani mashauri 400 mpaka 450 kwa mwaka, takwimu inaonesha kuwa kwa mwaka 2022 mashauri 450 yalisikilizwa na kuanzia Januari mpaka Mei 2023 jumla ya mashauri 275 yamefunguliwa huku uelekeo ukionesha kuwa mashauri yanaweza kufika hadi 500 kwa mwaka 2023.
Aidha kwa upande wa Mahakama ya Mwanzo Mang’ula Mhe. Ngwembe alimweelekeza kwa Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo,Mhe. Adolph Majalibu kutumia nguvu kazi toka Magereza kuchimba barabara inayoingia katika jengo la Mahakama hiyo ili itakapokamilika na kufunguliwa iwe rahisi kuingia pia hakusita kutoa pongezi zake kwa uongozi wa juu wa Mahakama kwa kujenga jengo hilo zuri ambalo limekamilika kwa hatua kubwa.
Majalibu alisema Mahakama ya Mwanzo Mang’ula inasikiliza takribani mashauri 300 mpaka 350 kwa mwaka. Inahudumia wananchi toka kata nne na takwimu inaonesha kuanzia mwezi Januari mpaka mwezi Mei 2023 jumla ya mashauri 164 yamefunguliwa.
Mhe. Ngwembe aliambatana na Naibu Msajili Mhe. Augustina Mbando, Mtendaji wa Mahakama Ahmed Ng’eni wote wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Morogoro.
Ukagu6zi wa jengo la Mahakama ya Mwanzo Mlimba unaendelea.
Matenki ya kuhifadhia maji katika jengo la Mahakama ya Mwanzo Mang’ula.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni