Na Stephen Kapiga-Mahakama Mwanza.
Madalali na Wasambaza yaraka za Mahakama ya Tanzania wa Mkoa wa Mwanza hivi karibuni waliendesha mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa Udhibiti wa Madalali na Wasambaza Nyaraka wa Mahakama ‘court broker and process server management system’ mafunzo yaliyofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC), Mwanza.
Akiendesha mafunzo hayo Katibu wa Madalali na Wasambaza Nyaraka wa Mahakama Mkoa wa Mwanza Bw. Nehemia Nyadhi alisema mafunzo yana umuhimu kwa wadau hao wa Mahakama ili kuwawezesha kuendeana na kasi ya matumizi ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) ndani ya Mahakama ya Tanzania.
”Ndugu zangu nipende tu kuwajulisha kuwa kupitia mfumo huu madali na wasambaza nyaraka wote watasajiliwa na kutambulika rasmi kupitia mfumo na hivvo kuiwezesha Mahakama kuwatumia Madali na Wasambaza Nyaraka walio rasmi” alisema Nyadhi.
Aidha alisema mafunzo hayo kwa ngazi ya Taifa yalifanyika Mkoani Arusha ambapo kila Mkoa ulitoa mwakilishi kwa upande wa Madali na Wasambaza Nyaraka ambaye ndiye aliyekuwa dalali mkufunzi kwa kila Mkoa wake husika.
Nyadhi aliongeza kwamba kutumika kwa mfumo huo kutaweza kuwasidia wananchi na wadau wa Mahakama kuweza kuwatambua wote waliosajiliwa na Mahakama ya Tanzania.Mbali na hilo pia itawawezesha kuweza kujisajili mara tu wanapokuwa wamelipia ada yao ya kila mwaka ya utendaji kazi inayoifanya Mahakama kuwapa kazi wale waliohuhisha leseni zao na kuondokana vishoka.
Kuanza kazi kwa mfumo huo , inaashiria kuwa ndani ya Mahakama kwa sasa matumizi ya TEHAMA hayakwepeki tena kwani kila mdau wa ameunganishwa na mfumo wa wenye lengo la kumsaidia kupunguza gharama na muda ili kupata huduma za Mahakama.
Hivi sasa miongoni mwa mifumo ambayo inatumiwa na wadau wa Mahakama ni pamoja na ‘e-wakili’ mfumo wa kuwasajili na kuwatambua mawakili, mfumo wa kufungua mashauri kwa njia ya kielektroniki ‘e-case filing . ‘ambao unawawezesha wadau kusajili mashauri yao wakiwa ndani ya ofisi zao au majumbani mwao pasipo kuwa na haja ya kufika mahakamani, mfumo wa kuendesha mashauri kwa njia ya video ‘visual court’ maalumu kwa kuendesha mashauri kwa njia video baina ya Jaji wa Mahakama au Hakimu pamoja na wadaawa wakiwa katika maeneo yao.
Katibu wa Madalali na Wasambaza Nyaraka Mkoa wa Mwanza Bw. Nehemia Nyadhi (kushoto)akiwasilisha mada kwa wadau hao(hawapo pichani) wakati wa mafunzo ya mfumo wa Udhibiti wa Madalali na Wasambaza Nyaraka za Mahakama yaliyofanyika hivi karibuni katika ukumbi wa mikutano wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC),Mwanza.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni