Afisa Kumbukumbu wa Mahakama ya Tanzania, Bi. Mariam Jacob (aliyesimama) akitoa maelezo ya jinsi kujaza fomu ya orodha ya mali za marehermu kwa Bi. Mwajabu Difika(aliyevaa ushungi wa maruni) na Bi. Mwasha Rashid ndani ya Mahakama Inayotembea iliyopo banda la Mahakama ya Tanzania kwenye Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (SabaSaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius K. Nyerere, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Hakimu Mkazi wa Mahakama Inayotembea,Mhe. Simon Laizer akisaini fomu hiyo.
Hakimu Mkazi wa Mahakama Inayotembea,Mhe. Simon Laizer akitoa maelezo kuhusu fomu ya mgawanyo wa mali za marehemu kwa wananchi waliofika kupata huduma hiyo(hawapo pichani)
Mawakili kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika(TLS) Chapter ya Ubungo wakitoa huduma ya kiapo cha kutokuwa na ajira kwa Bi. Zawadi Selemani(kulia) na (kulia aliyevaa nguo nyeusi) ni Bi. Oliver Katamwa kwenye banda la Mahakama ya Tanzania katika maonesho hayo.
Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Watoto Kisutu, Mhe. Orupa Mtae akisikiliza maelezo kutoka kwa Bw. Martin Kamisha(aliyenyoosha mkono) ambaye anataka kufahamu taratibu za kuasili mtoto kwenye banda la Mahakama ya Tanzania katika maonesho hayo.
Hakimu Mkazi Mwandamizi kutoka Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki (IJC) , Temeke cha Masuala ya Familia akitoa elimu kuhusu masuala ya mirathi kwa wananchi waliofika kwenye Kituo hicho kilichopo katika banda la Mahakama ya Tanzania.
(Picha na Magreth Kinabo- Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni