Jumatano, 28 Juni 2023

MAHAKAMA YA TANZANIA YASHIRIKI MAONESHO YA BIASHARA YA KIMATAIFA 'SABASABA'

JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

MAHAKAMA YA TANZANIA


                                                                                           
                                                        
TANGAZO

MAHAKAMA YA TANZANIA INAPENDA KUWATAARIFU WANANCHI NA WADAU WOTE KWA UJUMLA KUWA INASHIRIKI KATIKA MAONESHO YA 47 YA BIASHARA YA KIMATAIFA ‘SABASABA’ KUANZIA TAREHE 28 JUNI, 2023. KATIKA KIPINDI CHA MAONESHO HAYO, MAHAKAMA ITATOA HUDUMA ZIFUATAZO: -

1. HUDUMA YA KUSIKILIZA MASHAURI MAHAKAMA INAYOTEMBEA ‘MOBILE COURT SERVICES’

2. KUTOA ELIMU KUHUSU MATUMIZI YA TEHAMA MAHAKAMANI NA SAFARI YA MAHAKAMA KUELEKEA MAHAKAMA MTANDAO ‘e-JUDICIARY’. 

3. ELIMU KUHUSU HUDUMA NA TARATIBU MBALIMBALI ZA UFUNGUAJI WA MASHAURI YAKIWEMO MASHAURI YA MIRATHI.

4. KUELEZEA MFUMO ULIOBORESHWA WA KUSAJILI, KURATIBU NA KUSIMAMIA UENDESHAJI WA MASHAURI (ADVANCED CASE MANAGEMENT SYSTEM).

5.KUTOA ELIMU KUHUSU MASUALA YA NDOA, WOSIA NA MIRATHI.

6. KUELEZA HUDUMA ZINAZOTOLEWA NA NGAZI MBALIMBALI ZA MAHAKAMA IKIWEMO DIVISHENI ZA MAHAKAMA KUU

7. KUTOA ELIMU KWA WANANCHI KUTAMBUA UMUHIMU WA KUTUMIA KITUO CHA HUDUMA KWA WATEJA ‘CALL CENTRE’ YA MAHAKAMA YA TANZANIA KUTOA MALALAMIKO NA MAONI YAO.

8. KUTOA FOMU ZA UDAHILI NA KUZIPOKEA AMBAPO HUDUMA HII INATOLEWA NA CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA (IJA) LUSHOTO.

9. MSAADA WA KISHERIA ‘TLS’

AIDHA; KATIKA MAONESHO HAYO MAHAKAMA YA TANZANIA IPO KATIKA BANDA MOJA PAMOJA NA BAADHI YA WADAU WAKE AMBAO NI CHUO CHA UONGOZI WA MAHAKAMA (IJA) LUSHOTO, CHAMA CHA WANASHERIA TANGANYIKA (TLS), CHAMA CHA MAJAJI WANAWAKE TANZANIA (TAWJA), KITUO CHA SHERIA NA HAKI ZA BINADAMU (LRHC), ‘LAW SCHOOL OF TANZANIA’ NA WENGINE AMBAO WOTE WANATOA ELIMU KUHUSU MAENEO YAO.

HUDUMA TAJWA ZINATOLEWA NDANI YA BANDA LA MAHAKAMA, LILILOPO MKABALA NA BANDA LA JKT KATIKA VIWANJA VYA MWALIMU NYERERE ‘SABASABA’ BARABARA YA KILWA JIJINI `DAR ES SALAAM.

HUDUMA HIZO ZIMEANZA KUTOLEWA KUANZIA TAREHE 28 JUNI HADI JULAI 08, 2023.

EWE MWANANCHI, KARIBU UPATE ELIMU YA SHERIA PAMOJA NA KUTOA MAONI YAKO ILI KUBORESHA HUDUMA YA UTOAJI HAKI NCHINI.

WOTE MNAKARIBISHWA.

IMETOLEWA NA; 


Artemony T. Vincent,

MKUU WA KITENGO CHA HABARI, ELIMU NA MAWASILIANO,

 MAHAKAMA YA TANZANIA.

Muonekano wa Banda la Maonesho la Mahakama ya Tanzania linalopatikana mkabala na banda la Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) ndani ya Viwanja vya Mwalimu Nyerere almaarufu 'Sabasaba'.






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni