Jumatatu, 24 Julai 2023

JAJI MFAWIDHI SHINYANGA AANZA KAZI KUONANA NA WADAU

· Amtembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa

·Mkuu wa Mkoa aahidi ushirikiano 

Na Emmanuel Oguda-Mahakama, Shinyanga 

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Shinyanga, Mhe. Frank Mahimbali, Ijumaa tarehe 21 Julai, 2023, alimtembelea Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Christina Mdeme kwa lengo la kujitambulisha baada ya kuteuliwa hivi karibuni kushika wadhifa huo. 

Mhe. Mahimbali aliambatana na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Shinyanga, Mhe. Warsha Ng’humbu, Mtendaji wa Mahakama, Bi. Mavis Miti pamoja na Msaidizi wa Sheria wa Jaji, Mhe. Dushi Lugoye. 

Akiwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa, Jaji Mfawidhi alimweleza mwenyeji wake lengo la ujio wake, ikiwemo kujitambulisha kwake, kufahamiana na kuonana na uongozi wa Mkoa. 

Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa alimpongeza Mhe. Mahimbali kwa kuteuliwa kuwa Jaji Mfawidhi na kuahidi kutoa ushirikiano kwake na Mahakama kwa ujumla katika mambo mbalimbali.

Mhe. Mdeme alimkaribisha Jaji Mahimbali mkoani Shinyanga na kumtakia kila la kheri katika utekelezaji wa majukumu yake mapya.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Shinyanga, Mhe. Frank Mahimbali (kulia) akisalimiana na Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Christina Mdeme baada ya kuwasili ofisini kwake.

 

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Shinyanga, Mhe. Frank Mahimbali akiwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Christina Mdeme, akisisitiza jambo wakati Jaji Mfawidhi alipomtembelea ofisini kwake.

Naibu Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Shinyanga, Mhe. Warsha Ng’humbu akiwa katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa Shinyanga.

Mtendaji wa Mahakama, Bi. Mavis Miti akiwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa.

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Mhe. Christina Mdeme akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Shinyanga, Mhe, Frank Mahimbali (kulia), Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Shinyanga, Mhe. Warsha Ng’humbu (wa pili kushoto), Mtendaji wa Mahakama Bi. Mavis Miti (wa kwanza kulia) na Msaidizi wa Sheria wa Jaji Mhe. Dushi Lugoye (wa kwanza kushoto). 

(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni