Jumatatu, 24 Julai 2023

JAJI MKUU AIFARIJI FAMILIA YA ALIYEKUWA JAJI MKUU WA KWANZA MTANZANIA

 Na Magreth Kinabo -Mahakama

 

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma leo tarehe 24 Julai, 2023 ameitembelea familia aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania wa Kwanza Mtanzania, Hayati Augustine Bwanachila Saidi kwa ajili ya kuipa pole kufuatia kifo cha mama yao mzazi, Bi. Elizabeth Augustine Saidi.

 

Bi. Elizabeth Agustine Saidi alifariki dunia tarehe 21Julai, 2023 jijini Dar es Salaam.

 

Mhe. Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamis Juma aliitembelea familia hiyo nyumbani kwa marehemu Msasani Mikoroshini jijini Dar es Salaam na kuwapa pole ndugu ,jamaa na marafiki.

 

Akizungumzia kuhusu msiba huo, mtoto wa marehemu, Bw. Daniel Saidi amesema misa na heshima za mwisho za kumwuaga mama yake  zitafanyika siku ya Jumatano, tarehe 26, Julai2023 katika Kanisa la Katoliki la Parokia ya Mtakatifu Petro (St. Peters), Osterbay, kuanzia saa 6 mchana hadi saa 9 alasiri . Kisha mwili wa marehemu utasafirishwa kwenda Marangu Moshi kwa mazishi.

 

Mazishi ya mama Elizabeth Augustine Saidi yatafanyika siku ya Alahamisi tarehe 27 Julai, 2023 saa saba mchana nyumbani kwake Nduweni Marangu, Moshi.

 

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akimpa pole Bw. Daniel Saidi  ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania wa Kwanza Mtanzania, Hayati Augustine Bwanachila Saidi kufuatia kifo cha mama yake mzazi, Bi. Elizabeth Augustine Saidi, mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Msasani Mikoroshini leo tarehe 24 Julai, 2023 jijini Dar es Salaam.

Jaji Mkuu wa Tanzania,Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akisaini kitabu cha maombolezo ya kifo cha mke wa aliyekuwa  Jaji Mkuu wa Tanzania wa Kwanza Mtanzania, Hayati Augustine Bwanachila Saidi , Bi. Elizabeth Augustine Saidi mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Msasani Mikoroshini jijini Dar es Salaam.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akiwapa pole wadogo wa   mke wa  aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania wa Kwanza Mtanzania, Hayati Augustine Bwanachila Saidi kufuatia kifo cha dada yao  Bi. Elizabeth Augustine Saidi, mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Msasani Mikoroshini jijini Dar es Salaam.

 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.  Prof. Ibrahim Hamis Juma akimpa pole Jenerali Mstaafu, Fara Mohamed   ambaye ni mjomba wa aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania wa Kwanza Mtanzania, Hayati Augustine Bwanachila Saidi kufuatia kifo cha Bi. Elizabeth Augustine Saidi, mara baada ya kuwasili nyumbani kwa marehemu Msasani Mikoroshini jijini Dar es Salaam.

Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma akimpa pole mjukuu wa kwanza wa aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania wa Kwanza Mtanzania, Hayati Augustine Bwanachila Saidi, Bi. Sharon Prosper kufuatia kifo cha Bibi  yake  Bi. Elizabeth Augustine Saidi.

Picha juu nna chini ni  baadhi ya waombolezaji wakiwa katika msiba huo.


Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma(wa tatu kushoto) akizungumza na familia ya aliyekuwa  Jaji Mkuu wa Tanzania wa Kwanza Mtanzania, Hayati Augustine Bwanachila Saidi kufuatia kifo chamama yao, Bi. Elizabeth Augustine Saidi.

 Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe.  Prof. Ibrahim Hamis Juma (wa pili kulia) akizungumza jambo na Jenerali Mstaafu, Fara Mohamed, ambaye ni mjomba wa  aliyekuwa Jaji Mkuu wa Kwanza Tanzania, Hayati Augustine Saidi. 


(Picha na Magreth Kinabo- Mahakama)

 

 

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni