Alhamisi, 6 Julai 2023

JAJI MLYAMBINA ATEMBELEA BANDA LA MAHAKAMA SABA SABA

Na Mwanaidi Msekwa-Mahakama ya Kazi

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi, Dkt. Yose  Mlyambina leo tarehe 6 Julai, 2023 ametembelea Banda la Mahakama ya Tanzania katika Maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (SabaSaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.

Mhe. Dkt. Mlyambina ambaye aliambatana na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi, Mhe. Enock Matembele alipokelewa na Naibu Msajili Masjala Kuu. Mhe. Hussein Mushi na alipata fursa ya kujifunza masuala mbalimbali ya kisheria kutoka kwa wataalam waliopo katika Banda hilo.

Katika ziara yake, Jaji Mfawidhi alipendelea kufahamu takwimu za wadau wanaofika Banda la Mahakama na maswali muhimu yanayoulizwa ili kutoa fursa zaidi katika maboresho yanayoendelea mahakamani.

Jaji Mfawidhi pia alikutana na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Camillius Wambura ambaye alitembelea Banda la Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi na kueleza ongezeko la kasi ya usikilizaji wa mashauri ya kazi.

Amesema hadi kufikia leo tarehe 06 Julai, 2023, mashauri ya kazi 620 yalifunguliwa na mashauri 718 kumalizika na mashauri 321 yanaendelea mbele ya Majaji watatu na Naibu Wasajili wawili.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi, Dkt. Yose  Mlyambina (kushoto) akiingia katika Banda la Mahakama ya Tanzania alipotembelea leo tarehe 6 Julai, 2023 maonyesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (SabaSaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam. Kulia ni Naibu Msajili katika Divisheni hiyo, Mhe. Enock Matembele.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi, Dkt. Yose  Mlyambina akiwa katika banda la Masjala Kuu.


Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi, Dkt. Yose  Mlyambina akiwa katika banda la Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA).


Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi, Dkt. Yose  Mlyambina akiwa katika banda la Usuluhishi.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi, Dkt. Yose  Mlyambina akiwa katika banda la Maktaba.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi, Dkt. Yose  Mlyambina akiwa katika banda la Mahakama Kuu, Divisheni ya Biashara.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi, Dkt. Yose  Mlyambina akiwa katika banda la Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi, Dkt. Yose  Mlyambina akiwa katika banda la Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Kazi, Dkt. Yose  Mlyambina akisalimiana na Mkuu wa Jeshi la Polisi, IGP Camilus Wambura walipokutana kwenye banda la Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi. 
(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni