Na Magreth Kinabo-Mahakama
Msimamizi wa Kituo cha Huduma kwa Mteja cha Mahakama ya Tanzania, ambaye ni Hakimu Mkazi Mwandamizi, Mhe. Denice Mlashani amesema tangu kituo hicho kianzishwe kimepokea mirejesho 2,444 na kushughulikia mirejesho 2,429 sawa na asilimia 99.38.
Mhe. Mlashani ameyasema hayo leo tarehe 04 Julai, 2023 wakati Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania alipotembelea banda la Mahakama ya Tanzania lililopo katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa (SabaSaba) yanayoendelea katika Viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam.
Mhe. Mlashani amesema Kituo hicho ambacho kilianzishwa tarehe 01 Machi, 2022, malengo yake ni kupokea maoni, malalamiko na mapendekezo kutoka kwa wananchi juu ya huduma za mahakama kwa kupiga namba ya simu au kutuma ujumbe mfupi wa maandishi.Alizitaja namba zinatumika katika Kituo hicho ni 0752500400 au 0739502401.
“Hakuna malalamiko ya nakala za hukumu kwa sababu zinatolewa kupitia mtandao wa Tanzilii, ufunguajin wa mashauri kwa kutumia mtandaon umesaidia kupunguza tatizo la rushwa na upatikanaji wa nyaraka mbalimbali,”amesema Mhe. Mlashani.
Ameongeza kwamba usikilizaji nwa mashauri kwa njia ya mtandao (video conference) Mahakama Inayotembea umepunguza malalamiko ya ucheleweshaji wa mashauri mahakamani, uelimishaji wa kamati za maadili kuanzia ngazi ya Wilaya na Mkoa pia umepunguza kwa kiasi kikubwa malalamiko ya maadili ya maafisa wa Mahakama na kuwepo kwa miongozo mbalimbali na elimu kswa mahakimu juu ya dhamana.
“Tumebakiza maeneo machache yanayolalamikiwa na wadau wa Mahakama ambayo ni utekelezaji wa maamuzi kuchukuua muda mrefu, yakiwemo malipo ya mirathi,” amesisitiza.
Hakimu huyo alifafanua kuwa, sababu zinazochelewesha utekelezaji wa maamuzi kuwa ni wadaawa kuchukua muda mrefu kwenda mahakamani kuomba utekelezaji wa maamuzi, wadaawa kuwa na mapingamizi yasiyo kuwa na msingi na Mawakili kushindwa kuwaongoza vizuri wateja wao katika hatua ya utekelezaji wa maamuzi.
Kwa upande wake Mtendaji huyo, akizungumza mara baada ya kutembelea banda hilo amewaomba wananchi kuiamini Mahakama na kutumia nafasi ya kupata elimu juu ya masuala mbalimbali ya kisheria vizuri inayotolewa na vyombo vya habari kwa kuwa Mhimili huo unatumia gharama kubwa kutoa elimu hiyo.
MATUKIO KATIKA PICHA-ZIARA YA MTENDAJI MKUU WA MAHAKAMA YA TANZANIA, PROF. ELISANTE OLE GABRIEL KATIKA BANDA LA MAHAKAMA YA TANZANIA LINALOSHIRIKI KATIKA MAONESHO YA 47 YA KIBIASHARA YA KIMATAIFA, 'SABASABA', 2023.
Mtendaji Mkuu, Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Mahakama ya Tanzania leo tarehe 4 Julai, 2023. Mahakama ya Tanzania inashiriki katika maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa ‘Sabasaba’, 2023.
Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi Mipango- Mahakama ya Tanzania, Bi. Gladys Qambaita aliyekuwa akimueleza kuhusu mipangio na maboresho mbalimbali ya Mhimili huo.
Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akisaini kitabu cha wageni alipotembelea banda la Mahakama Kuu Masjala Kuu lililopo ndani ya banda kuu la Mahakama ya Tanzania katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa 'Sabasaba', 2023.
Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akipata maelezo kutoka kwa Wakurugenzi Wasaidizi Kurugenzi ya Usimamizi wa Mashauri Mahakama ya Tanzania. Kushoto ni Mhe. Moses Ndelwa na kushoto kwake ni Mhe. Hawa Mnguruta.
Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akipata maelezo kutoka kwa Maafisa kutoka Kituo cha Huduma kwa Mteja (Call Centre) ya Mahakama. Kulia ni Mhe. Denice Mlashani na kushoto ni Bi. Evetha Mboya.
Prof. Ole Gabriel akipata maelezo kutoka Banda la Kurugenzi ya Usimamizi, Ukaguzi wa Huduma za Mahakama, Maadili na Malalamiko. Kulia ni Hakimu Mkazi Mwandamizi anayehudumu katika Kurugenzi hiyo, Mhe. Lome Mwapemela.
Maelezo kutoka Mhe. Orupa, Hakimu Mahakama ya Watoto-Temeke.
Maelezo kutoka Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi.
Mtendaji Mkuu akiwa katika banda la Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) ambao ni moja ya Wadau waliopo ndani ya banda la Mahakama ya Tanzania mkabala na banda la JKT lililopo ndani ya Viwanja vya Mwalimu Nyerere ‘Sabasaba’ jijini Dar es Salaam.
(Picha na Mary Gwera, Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni