Jumatano, 30 Agosti 2023

BONANZA LA JMAT MKOA WA DAR ES SALAAM KUFANYIKA VIWANJA VYA GYMKHANA

 Na Magreth Kinabo-Mahakama

Mwenyekiti wa   Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT) wa tawi la Mahakama ya Rufani Tanzania, Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye ni Jaji wa Mahakama hiyo,Mhe. Shabani Lila amesema Bonanza maalum la michezo mbalimbali lililoandaliwa na JMAT mkoa wa Dar es Salaam litafanyika katika Viwanja vya Gymkhana vilivyoko jijini Dar es Salaam. 

 

Akizungumza katika kikao cha kikao cha Kamati ya Maandalizi ya Bonanza hilo, Mhe. Jaji Lila, ambaye ni Mwenyekiti wa maandalizi hayo kilichofanyika jana tarehe 30, Agosti, 2023 jioni  amesema mabadiliko ya viwanja vya awali vya Shule ya Sheria (Law School) yamefanyika kutokana na sababu viwanja hiyo vitakuwa na matumizi mengine. 

 

Mhe. Jaji Lila ameongeza kuwa mazoezi kwa ajili ya michezo tofauti yanaendelea na amewataka Majaji Wafawidhi, Mahakimu Wafawidhi na Watendaji wa   Mahakama za Mkoa huo, kuhamasisha wanachama na watumishi wa Mahakama ya Tanzania kutoka katika kuendelea kujitokeza kushiriki ili kuwezesha Bonanza hilo kufana.

 

Baadhi ya michezo itakayochezwa katika Bonanza hilo ni mpira wa miguu na pete,kuvuta kamba, kukimbiza kuku, kukimbia na gunia, bao, draft, kukimbia mita 100 na mita 400 na kuendesha baiskeli mwendo wa polepole na rede.

 

Kikao hicho kilishirikisha viongozi wa matawi matatu ya JMAT kutoka, Mahakama ya Rufani Tanzania, Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu na Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Majaji Wafawidhi, Mahakimu Wafawidhi, wakiwemo wajumbe wengine kutoka utawala. 

 

Bonanza hilo litafanyika tarehe 9 Septemba, 2023 kwenye viwanja hivyo na ratiba kamili  ya shughuli mbalimbali itatolewa baadae.

Mwenyekiti wa   Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT) wa tawi la Mahakama ya Rufani Tanzania,Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Jaji Shabani Lila(kulia) akizungumza jana tarehe 30, Agosti, 2023 kuhusu maandalizi hayo.Kushoto ni Mwenyekiti wa JMAT Mkoa huo tawi la Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu, Mhe. Jaji Latifa Mansoor.

Mwenyekiti wa JMAT Mkoa huo tawi la Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu, Mhe. Jaji Latifa Mansoor akifafanua jambo.

                      Majaji Wafawidhi wakiwa katika kikao hicho.
Wajumbe wa wakiwa katika kikao hicho.
Wajumbe.
 Sekretarieti ikiratibu kikao hicho.

 

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni