Jumatano, 30 Agosti 2023

WANANCHI 182 WAPATIWA ELIMU YA USULUHISHI MWEZI AGOSTI MWAKA HUU

 Na Sade Soka - Mahakama (UDSM) 

 

Jumla ya wananchi 182 waliofika kupata huduma za Mahakama katika Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi na Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, wamepatiwa elimu juu ya utatuzi wa migogoro kwa njia ya usuluhishi katika kipindi cha mwezi Agosti, 2023.

 

Akizungumza na Kitengo cha Habari, Elimu na Mawasiliano cha Mahakama ya Tanzania leo tarehe 30 Agosti, 2023 Hakimu Mkaziwa Kituo cha Usuluhishi, Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Mohamed Burhani amesema wamekuwa wakitoa elimu  hiyo kwenye eneo la Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi iliyopo jijini Dar  es Salaam ikiwa ni utaratibu wao wa kila Jumatano ya wiki.

 

Aidha Mhe. Burhani amewaambia  wananchi waliohudhuria mahakamani hapo, kuwa kwa kutumia  njia ya usuluhishi, hutumia muda wa siku 30 tu katika kusuluhisha kesi zinazoletwa na ikitokea usuluhishi umefanikiwa kesi hiyo inakuwa imeisha, na huisha kwa makubaliano kutoka pande zote mbili.

 

“Kazi yetu sisi ni usuluhishi, tunasuluhisha mashauri yaliyofunguliwa Mahakamani, kwa mashauri ambayo yameanzia Mahakamani hapa kwa maana kwamba Mahakama Kuu Divisheni ya Ardhi na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam,” amesema Mhe. Burhani.

 

Aidha Mhe. Burhani amefafanua kwamba malengo ya kutoa elimju hiyo ni  kuwawezesha wananchi kukifahamu Kituo hicho, ikiwemo njia hiyo, kufahamu huduma zinazopatikana na kujua haki za za msingi.

 

Pia aliwaambia usuluhishi huu unafaida kubwa kwa sababu hutunza muda, kwani kukata shauri kwenye Mahakama ya kwaida huchukua muda mrefu tofauti na kukata shauri katika Kituo hicho.Na mwisho wa usuluhishi inakuwa wote wameshinda kesi.  

 

Hakimu Mkazi wa Kituo hicho, Mhe Mohamed Burhani (aliyesimamama)akitoa elimu hiyo kwa wananchi waliofika mahakamani hapo. 

 Zulpha Ramadhan akigawa vipeperushi kwa mmoja wa wananchi waliopatiwa elimu hiyo, huku Hakimu Mkazi,Mhe Mohamed Burhani akitoa elimu.


 Mchungaji  Praseda Rutehangwa akisoma moja ya vipeperushi vilivyogaiwa wakati wa utoaaji elimu hiyo usuluhishi.


Baadhi ya wananchi waliohudhuria katika elimu ya usuluhishi wakipitia vipeperushi mbalimbali vilivyotolewa. 

 

Wananchi wakiwa wanamsikiliza. elimu ya  usuluhishi.


(Picha na Sade Soka -UDSM).

 

(Habari hii imehaririwa na Magreth Kinabo-Mahakama) 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni