Na Sade Soka- Mahakama (UDSM)
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe Mustapher Mohamed Siyani, amehimiza umuhimu wa mazoezi kwa watumishi wote wa Mahakama ya Tanzania.
Alitoa tamko hilo jana jioni tarehe 22 Agosti ,2023 katika Viwanja vya Shule ya Sheria (law school) vilivyopo jijini Dar es salaam, wakati wa maandalizi ya Bonanza maalum lilioandaliwa na Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT) Mkoa wa Dar es salaam litakalofanyika tarehe 9 septemba 2023.
Mhe. Jaji Kiongozi, amesema kwamba watumishi hao wanatakiwa kushiriki kwa sababu wao ni familia moja na michezo ni muhimu kwa sababu wanatumia muda mwingi kukaa mahakamani wanapotimiza majukumu yao ya kila siku.
Aliongeza kuwa michezo ina uhimarisha afya inatufanya tuweze kutimiza majukumu yetu ya kila siku vizuri.
“Michezo inaimarisha afya, na afya inaweza kufanya hutimize majukumu yetu. Bila afya hatuwezi kutimiza majukumu ambayo taifa letu limetupa sisi tufanye na sisi tulifanyie na jukumu pekee tulilonalo sisi ni kutoa haki, kwa Watanzania,” amesisitiza Mhe. Jaji Kiongozi Siyani.
Aliwataka watumishi wa Mahakama kushiriki kwenye mazoezi hayo wafike bila kukosa kwa manufaa ya afya zao na kuwaahidi atakuwa akishiriki kila atakapopata nafasi.
Aidha Jaji Kiongozi huyo amempongeza Mwenyekiti wa Kamati ya Maandilizi ya Bonanza hilo, Mhe. Shabani Lila, ambaye ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, pia Mwenyekiti wa JMAT tawi la Mahakama hiyo Mkoa wa Dar es Salaam kwa kuliandaa ambalo litawakutanisha watumishi wote wa eneo hilo na kuimarisha umoja. Pia alishauri suala hilo liwe endelevu.
bluu) ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama ya Kuu ya Tanzania, Kituo cha Usuluhishi, Mhe. Zahra Maruma na (mwenye tisheti nyekundu) ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi, Mhe. Kevin Mhina.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani akiendesha baiskeli kwa mwendo wa polepole.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama ya Kuu ya Tanzania, Kituo cha Usuluhishi, Mhe. Zahra Maruma akifunga goli katika mchezo wa mpira wa pete kwenye mazoezi hayo.
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani akipiga danadana 100, huku akishuhudiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT) wa tawi la Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Shabani Lila, (kushoto).
Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani(kushoto) akicheza mchezo wa bao na Hakimu Mkazi na Mwenyekiti wa JMAT tawi la Mahakama Kuu Masjala Kuu, Mhe. Mary Kallomo(kulia).
(Picha na Magreth Kinabo- Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni