Jumamosi, 5 Agosti 2023

JAJI MFAWIDHI MUSOMA AFANYA ZIARA

Na Francisca Swai – Mahakama, Musoma.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya hivikaribuni alifanya ziara ya kikazi katika Mahakama mbalimbali kukagua shughuli za kimahakama na kuongea na watumishi.

Katika ukaguzi huo, Mhe. Mtulya aliambatana na Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Musoma, Mhe. Frank Moshi na Mtendaji wa Mahakama Kuu Musoma, Bw. Festo Chonya.

Akiongea na watumishi katika ziara yake, Jaji Mfawidhi aliwaasa kufanya kazi kwa moyo, uadilifu, weledi na uwajibikaji ili kufikia malengo yaliyowekwa na Kanda hiyo pamoja na Mahakama ya Tanzania kwa ujumla.


Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya (aliyenyoosha mkono) akieleza jambo kuhusu tenki la kuvuna maji lililoko katika Mahakama ya Mwanzo Mtana.

Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Rorya, Mhe. Tumaini Marwa (aliyenyoosha mkono) akielezea jambo kuhusu mazingira na zoezi la upandaji miti katika Mahakama hiyo.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya (katikati), akikagua mazingira katika Mahakama ya Wilaya Butiama na kumpongeza Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo, Mhe. Judith Semkiwa (wa pili kulia) kwa kazi nzuri na upandaji wa miti ya matunda.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Musoma Mhe. Fahamu Mtulya (mwenye tai nyekundu), akishiriki katika zoezi la utambuaji wa mipaka ya Mahakama ya Mwanzo Mcharo iliyoko wilayani Bunda wakati wa ziara yake. Utambuzi huo wa mipaka ulifanywa kwa ushirikiano na viongozi wa Mahakama Kuu Musoma, Mahakama ya Wilaya Bunda, Maafisa Ardhi kutoka Ofisi ya Mkurugenzi Bunda, Uongozi wa kijiji na wananchi wa eneo hilo.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya (katikati) akiongea na watumishi wa Mahakama ya Wilaya Tarime (hawako pichani) wakati wa ukaguzi katika Mahakama hiyo. Wengine ni Naibu Msajili Mahakama Kuu Musoma, Mhe. Frank Moshi (kushoto), Mtendaji wa Mahakama Kuu Musoma Bw. Festo Chonya (kulia).

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya (katikati) na viongozi aliambatana nao, Mtendaji wa Mahakama Kuu Musoma, Bw. Festo Chonya (wa nne kushoto), Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Tarime, Mhe. Veronica Selemani (wa tatu kulia), Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mwanzo Nyamongo, Mhe Julieth Rwegasira (wa nne kulia) wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Nyamongo iliyoko wilayani Tarime.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya (katikati) na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Mtana iliyoko wilayani Tarime.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya (katikati) na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama ya Wilaya Tarime.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya (katikati) na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama ya Wilaya Butiama.
Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya Musoma, Mhe. Aristida Tarimo (aliyesimama) akisoma taarifa ya utendaji kazi wa Mahakama ya Wilaya Musoma wakati Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya alipofanya kikao kilichojumuisha watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Musoma na Mahakama ya Wilaya Musoma.


Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya (katikati), akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Mahakama Kuu Musoma na watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Musoma Mjini.


Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya (katikati) pamoja na viongozi wengine wakiongea na watumishi wa Mahakama ya Wilaya Bunda (hawako pichani) wakati wa ukaguzi katika Mahakama hiyo.
Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Musoma, Mhe. Fahamu Mtulya (katikati) na viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama ya Wilaya na Mahakama ya Mwanzo Bunda Mjini.

(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni