·Amtaka kuzingatia kiapo chake
Na Faustine Kapama,
Mahakama na Sade Soka (UDSM)
Jaji Mkuu wa Tanzania,
Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma leo tarehe 24 Agosti, 2023 amemwapisha Hakimu Mkazi,
Mhe. Langeni Robert kushika wadhifa huo.
Uapisho huo umefanyika
katika ofisi ya Jaji Mkuu iliyopo katika jengo la Mahakama ya Rufani jijini Dar
es Salaam na kuhudhuriwa na Viongozi mbalimbali, akiwemo Jaji Kiongozi wa Mahakama
Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani.
Viongozi wengine
waliohudhuria hafla hiyo ni Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert
Chuma, Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania-Divisheni, Bi. Mary Shirima, ambaye
alimwakilisha Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania na Msajili wa Mahakama Kuu
ya Tanzania, Mhe. Sharmillah Sarwatt.
Wengine ni Naibu Msajili
Mwandamizi wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Emmanuel Mrangu, Naibu
Msajili Mwandamizi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Arnold Kirekiano, Naibu Msajili Bernazitha
Maziku, Mtendaji wa Mahakama Maria Itala na wengine wengi.
Akizungumza katika hafla
hiyo fupi, Jaji Mkuu alimtaka Hakimu huyo mpya kuzingatia yale yote
aliyojifunza katika semina elekezi iliyotolewa kwa Mahakimu Wakazi 39 wapya hivi
karibuni katika Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto ili kuimarisha kiapo
chake.
“Kiapo chako cha leo ni
nyenzo muhimu kuliko yote kwa sababu kimetoa muhtasari kwa mambo muhimu ambayo
unatakiwa kuyafuata. Ukiweza kufuata kiapo chako hutapata changamoto ya aina
yoyote. Nikutakie kila heri katika kazi zako za uhakimu,” amesema.
Tarehe10 Agosti, 2023,
Jaji Mkuu aliwaapisha Mahakimu Wakazi 38 wapya na kuwataka kuwa huru, kuvumilia
na kujiepusha na upendeleo wowote ili kutekeleza kikamilifu jukumu la utoaji
haki kwa wananchi.
Aliwakumbusha Mahakimu
hao umuhimu walionao katika jamii kwa kuwa ndiyo wanaoshughulikia asilimia 70
ya mashauri yote yanayosajiliwa katika ngazi mbalimbali za Mahakama.
Mhe. Prof. Juma aliwahimiza
kuendeza zifa zilizopelekea wao kupata nafasi ya kuhudumu katika nafasi ya
Hakimu Mkazi, ikiwemo kuwa huru, kutokuwa na upendeleo, kuwa na uvumilivu, kusikiliza
ushahidi kwa makini na kutafakari kwa kina sheria kabla ya kufikia maamuzi.
Sehemu ya Viongozi waliohudhuria uapisho huo. Kutoka kulia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani, Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma, Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania-Divisheni, Bi. Mary Shirima, ambaye alimwakilisha Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania na Msajili wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sharmillah Sarwatt.
Viongozi mbalimbali wa Mahakama wakichukua kumbukumbu kadhaa wakati wa hafla ya kumwapisha Hakimu Mkazi, Mhe. Langeni Robert. Kutoka kulia ni Mtendaji wa Mahakama Maria Itala, Katibu wa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Aidan Mwilapwa na Katibu wa Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Mhe. Jovin Binshanga.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni