Jumatano, 6 Septemba 2023

JAJI LILA : AWATAKA WANA JMAT NA WATUMISHI WA MAHAKAMA YA TANZANIA KUHUDHURIA BONANZA

 Na Magreth Kinabo-Mahakama

Mwenyekiti wa  Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT) wa tawi la Mahakama ya Rufani Tanzania, Mkoa wa Dar es Salaam, ambaye ni Jaji wa Mahakama hiyo,Mhe. Shabani Lila amesema wanachama wa chama hicho, na watumishi wa Mahakama ya Tanzania watashiriki katika mazoezi ya pamoja kwenye Bonanza maalum la michezo mbalimbali lililoandaliwa na JMAT mkoa wa Dar es Salaam, ambalo litafanyika katika Viwanja vya Gymkhana vilivyoko jijini Dar es Salaam. 

 

Akizungumza katika kikao cha Kamati ya Maandalizi ya Bonanza hilo, Mhe. Jaji Lila, ambaye ni Mwenyekiti wa maandalizi hayo kilichofanyika jana tarehe 5 Septemba, 2023  jioni  amesema mazoezi hayo yataanza saa 12:00 asubuhi hivyo washiriki wanatakiwa kuwahi mapema kwenye viwanja hivyo.

 

Mhe. Jaji Lila ameongeza kuwa mazoezi kwa ajili ya michezo tofauti yanaendelea na amewataka Majaji Wafawidhi, Mahakimu Wafawidhi na Watendaji wa   Mahakama za Mkoa huo, kuhamasisha wanachama na watumishi wa Mahakama ya Tanzania  kuendelea kujitokeza kushiriki katika mazoezi hayo yanayoendelea ambayo siku ya Ijumaa tarehe 8 Septemba, 2023 yatafanyika kwenye viwanja hivyo badala ya vya Shule ya Sheria ili kuwezesha Bonanza hilo kufana.Pia  kamati ya maandalizi itakuwepo uwanjani hapo siku hiyo. 

 

Baadhi ya michezo itakayochezwa katika Bonanza hilo ni mpira wa miguu na pete,kuvuta kamba, kukimbiza kuku, kukimbia na gunia, bao, draft, kukimbia mita 100 na mita 400 na kuendesha baiskeli mwendo wa polepole na karata.Washindi katika  michezo hiyo watapatiwa kuku, vikombe na medali na wengine vyeti.


Kikao hicho ni cha tatu kufanya kwa ajili ya  kufanya tathimini ya mwenendo wa Bonanza hilo.



(Wahe. Majaji wakisikiliza hoja kwenye kikao cha Maandalizi ya Bonanza maalum lililoandaliwa na Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT), Mkoa wa Dar es Salaam litakalofanyika tarehe 9Septemba, 2023 kwenye Viwanja vya Gymkhana jijini, Dar es Salaam. Kikao hicho kilifanyika jana jioni tarehe 5 Septemba, 2023 katika ukumbi wa Mahakama ya wazi wa Mahakama ya Rufani Tanzania.

Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, ambaye pia ni Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni, Bi.Mary Shirima (kulia), akiwa katika kikao hicho, (kushoto) ni

Msajili wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Sylvester Kainda na (katikati) ni Afisa Tawala wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Bw. Ezra Kyando.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, Mhe. Salma Maghimbi (katikati) akichangia hoja kwenye kikao hicho.

Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Shabani Lila (wa pili kushoto) akiwa na  jezi wanachama wa JMAT na wachezaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania  wa mpita wa miguu na pete katika kikao hicho. Kulia ni Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kituo cha Usuluhishi, Mhe.  Zahra Maruma (wa pili kulia) akiwa  na jezi hizo kwa upande wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

 Sekretarieti na wajumbe wengine  wakiwa katika kikao cha Bonanza.

  

.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni