Jumatatu, 4 Septemba 2023

JAJI MFAWIDHI MTWARA ASHIRIKI MBIO ZA KOROSHO MARATHONI

Na. Richard Matasha-Mahakama, Mtwara.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mtwara, Mhe. Rose Ebrahim hivi karibuni alishiriki kikamilifu katika msimu wa pili wa mbio zinazoandaliwa na Bodi ya Korosho, maarufu kama “Korosho Marathon” zilizofanyika kwenye Viwanja vya Nangwanda mkoani hapa.

Awali, akiongea wakati anapokea mwaliko wa kushiriki kwenye mbio hizo, Jaji Mfawidhi alionyesha kufurahia tukio hilo kwa vile Mahakama ipo tayari kushirikiana na wadau wengine katika kuutangaza uchumi katika maeneo yote nchini.

“Kazi ya Mahakama siyo kufunga watu, bali ni kuinua maisha ya watu kiuchumu. Kama huku Mtwara, rasilimali yetu kubwa ni zao la korosho na sisi kama Mahakama tupo tayari kushirikiana nanyi ili kutangaza na kuinua uchumi wa wana Mtwara na Tanzania kwa ujumla,” alisema.

Mhe. Ebrahim alishiriki katika mbio za kilometa tano pamoja na Viongozi wengine wa Mahakama, akiwemo Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara, Mhe. Charles Mnzava na Mtendaji wa Mahakama Kuu Mtwara, Bw. Richard Mbambe.

Wengine ni Mahakimu Wakazi, Mhe. Alex Robert na Mhe. Baro Nyaki pamoja na watumishi wengine wa Mahakama.

Katika mashindano hayo, Mhe. Mnzava aliibuka mshindi wa kwanza wa kilometa tano. Hatua ya Viongozi na watumishi wa Mahakama inathibitia nia yao ya kuunga mkono na kuhamasisha mazoezi kwa wananchi kwa ujumla ili kutengeneza afya dhabiti.

Baadhi ya watumishi wa Mahakama walishiriki katika mbio za kilometa 10 na kilometa 21, hii yote imetokana na program ya ‘jogging’ ya kila siku ya Jumamosi inayofanywa kwa watumishi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mtwara.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara, Mhe. Rose Ebrahim (katikati) na viongozi wengine wakifurahia tunzo za medali walizotwaa baada ya kukamilisha mbio za Kilometa tano. Wengine ni Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara, Mhe. Charles Mnzava (kulia) na kushoto ni Mtendaji wa Mahakama Kuu Mtwara, Bw. Richard Mbambe.   

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mtwara, Mhe. Rose Ebrahim akiwa katika picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama Kanda ya Mtwara walioshiriki katika m bio za Korosho Marathon 2023.
Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara, Mhe. Charles Mnzava katika picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama Kanda ya Mtwara walioshiriki katika mbio za Korosho Marathon 2023.

Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mtwara, Mhe. Rose Ebrahim akipokea vifaa vya kushiriki mbio za Korosho Marathon kutoka mwakilishi wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo.
Naibu Msajili wa Mahakama Kuu, Kanda ya Mtwara, Mhe Fredrick Lukuna akipokea vifaa vya kushiriki mbio za Korosho Marathon kutoka mwakilishi wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo.

 

Hakimu Mfawidhi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Mtwara, Mhe Charles Mnzava akipokea vifaa vya kushiriki mbio za Korosho Marathon kutoka mwakilishi wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo.

 

Mtendaji wa Mahakama Kuu Mtwara, Bw. Richard Mbambe akipokea vifaa vya kushiriki mbio za Korosho Marathon kutoka mwakilishi wa kamati ya maandalizi ya mbio hizo.

(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama)

 


 


 


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni