Na. Mohamed Kimungu- Mahakama Songwe
Mahakama
ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Songwe kupitia kamati ya Elimu Mkoa imewatembelea wanachama
wa club ya Mahakama katika shule ya sekondari Ilolo kwa lengo la kutoa elimu kwa
wanafunzi hao.
Akitoa
elimu kwa wanaclub hao, Hakimu Mkazi Mwandamizi Mahakama ya Wilaya Mbozi na
Mwenyekiti wa kamati ya elimu Mkoa wa Songwe, Mhe. Vitalis Changwe alisema,
kwamba ni jukumu la Mahakama kutoa elimu kwa wanachama wa Club hiyo, kuilea, kuijengea
uwezo na kuitembelea kadri ya ratiba ilivyopangwa na Mahakama.
“Ni
wajibu wa kila mwanaclub kuhakikisha anatimiza ndoto yake hivyo club hii
itumike kama chachu ya kuendelea kuwajengea uwezo kimasomo na kuendelea
kujiimarisha ili siku moja mfaidi matunda ya hiki kitu mnachokifanya leo”,
aliongeza Mhe. Changwe
Wanafunzi
hao wamefurahishwa na elimu kuhusiana na sheria za Mirathi na Wosia iliyotolewa
na Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Mwanzo Mlowo Mhe. Mesia Gan’golo na Hakimu wa Mahakama
ya Mwanzo Vwawa Mhe. Martha Malima.
Aidha,
akizungumza kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Mwanafunzi Faraja Chilembe wa
kidato cha tatu katika shule hiyo aliupongeza Uongozi wa Mahakama ya Hakimu
Mkazi Songwe kwa jitihada kubwa za
kuanzisha club shuleni hapo na kuendelea kutoa elimu ya sheria “napenda
kuchukua nafasi hii kuwapongeza Mahakama ya Tanzania kwa kuendelea kuwatembelea
na kutoa elimu ya sheria kupitia club yetu tumefarijika kupata elimu ya wosia
na mirathi itatusaidia katika maisha yetu ya kila siku”, aliongeza Mwanafunzi
huyo.
Akihitimisha
zoezi hilo la utoaji elimu kwa Club ya Mahakama iliyopo Shule ya Sekondari
Ilolo, Mwenyekiti wa kamati ya Elimu Mkoa wa Songwe, Mhe. Vitalis Changwe aliwakabidhi
wanafunzi hao zawadi ya kalamu boksi nne (4) na kuwataka kushiriki kikamilifu
katika zoezi hilo la utoaji wa elimu na kuwa mabalozi wema ili kufikisha elimu
hiyo kwa familia zao na jamii inayowazunguka.
Hakimu Mahakama ya Mwanzo Vwawa mjini Mhe. Martha Malima akitoa Elimu kwa wanafunzi wa Shule ya Sekondari Ilolo mkoani Songwe kushoto ni Hakimu Mkazi Mwandamizi Mahakama ya Wilaya Mbozi na Mwenyekiti wa kamati ya elimu Mkoa wa Songwe, Mhe. Vitalis Changwe.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Ilolo wakimsikiliza kwa makini mtoa mada wa elimu ya sheria kuhusu wosia na Mirathi inayotolewa shuleni hapo.
Hakimu Mkazi Mahakama ya mwanzo Mlowo Mhe. Mesia Gan'golo (kulia) akitoa elimu kwa wanafunzi wa club ya Mahakama (hawapo pichani), wengine ni Hakimu Mahakama ya Mwanzo Vwawa mjini Mhe. Martha Malima (kushoto) na katikati ni Hakimu Mkazi Mwandamizi Mahakama ya Wilaya Mbozi na Mwenyekiti wa kamati ya elimu Mkoa wa Songwe, Mhe. Vitalis Changwe.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Ilolo wakimsikiliza kwa makini mtoa mada wa elimu ya sheria kuhusu wosia na Mirathi inayotolewa shuleni hapo.
Hakimu Mkazi Mwandamizi Mahakama ya Wilaya Mbozi na Mwenyekiti wa kamati ya elimu Mkoa wa Songwe, Mhe. Vitalis Changwe akifafanua jambo mbele ya wanafunzi wa club hiyo (hawapo pichani), wengine ni Hakimu Mahakama ya Mwanzo Vwawa mjini Mhe. Martha Malima (kushoto) na Hakimu Mkazi Mahakama ya mwanzo Mlowo Mhe. Mesia Gan'golo (kulia).
Hakimu Mkazi Mwandamizi Mahakama ya Wilaya Mbozi na Mwenyekiti wa kamati ya elimu Mkoa wa Songwe, Mhe. Vitalis Changwe akimkabidhi wanafunzi Faraja Chilembe zawadi ya kalamu boksi nne (4) kwa niaba ya wanaclub na kuwataka kushiriki kikamilifu katika zoezi hilo.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni