Na Hasani Haufi- Mahakama Songea
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Songea, Mhe. James Karayemaha hivi
karibuni alimtembelea Mkuu wa MKoa wa Ruvuma, Kanali Laban Thomas kwa ajili ya
kumsalimia na kujitambulisha.
Mkuu
wa Mkoa alionyesha kufurahishwa na kitendo hicho na kuahidi kumpa ushirikiano
ili aweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu kwani imekuwa desturi kwa Viongozi
wa Mahakama kumtembelea pindi wanapofika mkoani Ruvuma.
Kanali
Thomas alimweleza Jaji Mfawidhi kuwa maadili ya watumishi wa Mahakama yameimarika
kwani malalamiko kutoka kwa wananchi yamepungua kwa kiasi kikubwa kutokana na
uelewa wa huduma zinazotolewa mahakakani.
“Kupitia
elimu zinazotolewa kila siku na Mahakama Kanda ya Songea na pia kupitia vyombo
vya habari, wananchi wamekuwa na uelewa wa kutosha kuhusu huduma zinazotolewa
na wanajuwa mambo mengi kupitia jukwaa hili,” amesema.
Mkuu wa Mkoa alimwomba Jaji Mfawidhi kudumisha mahusiano mazuri yaliyopo kwani ushirikiano wa mihimili yote ya dola unasaidia kuimarisha utendaji, hivyo kuongeza imani ya wanachi ambao ndiyo wanufaika wakubwa wa huduma zinazotolewa.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Songea, Mhe. James Karayemaha akibadilishana
mawazo na Mkuu wa Mkoa Kanali Laban Thomas.
Picha
ya pamoja kati ya Jaji Mfawidhi (kulia) na Mkuu wa Mkoa.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Songea, Mhe. James Karayemaha (wa tatu kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Laban Thomas (wa tatu kushoto) pamoja na Viongozi wengine wa Mahakama.
Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Songea, Mhe. James Karayemaha(mwenye miwani) akiagana na Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma, Kanali Laban Thomas.
(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni