Na Magreth Kinabo-Mahakama na Sade Soka(UDSM)
Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Augustine Mwarija (ambaye ni M lezi wa Majaji wa Mahakama hiyo, ametoa ushauri kwa waandalizi wa Bonanza maalum la michezo mbalimbali lililoandaliwa na Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT) Mkoa wa Dar es Salaam, kuwa endelevu ili kuendeleza umoja na mshikamano katika utendaji kazi.
Mhe. Jaji Mwarija ametoa kauli hiyo leo tarehe 9 Septemba, 2023 alipokuwa mgeni rasmi kwa niaba ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma lililofanyika katika Viwanja vya Gymkhana vilivyoko jijini Dar es Salaam.
Akizungumzia kuhusu kauli mbiu ya Bonanza hilo, ‘Afya Imara, Mahakama Imara,” amesema ni kuhamasisha watumishi wa Mahakama kufanya mazoezi kupitia michezo mbalimbali ili kuhimarisha afya zao.
“Michezo husaidia kukabiliana na magonjwa yale yasiyoambukiza pamoja na yale yanayotokana na utendaji kazi wetu kwa sababu ya kukaa muda mrefuna kuandika kwa muda mrefu, nafarijika kati mwitikio ambao umeuonesha kwenye tukio hili, watumishi wa ngazi zote za Mahakama ya Tanzania hapa Dar es Salaam tumeweka historia ya kukutana hapa,” amesema Mhe. Jaji Mwarija.
Huku akisema inafaa jambo hilo lifanyike kila mwaka au zaidi.
Aidha Mhe. Jaji Mwarija ameongeza kwamba licha ya kucheza kutazana na kushangilia Bonanza hilo, kunajenga afya.
Aliwapongeza Majaji wa walioandaa Bonanza hilo, ambao ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Shabani Lila, ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Kuu, Mhe. Latifa Mansoor, Makamu Mwenyekiti, wahamasishaji na wote waliohusika kulifanikisha. Pia alishukuru taasisi mbalimbali na watu waliohusika katika Bonanza hilo.
Michezo iiliyochezwa katika Bonanza hilo ni mpira wa miguu na pete, kuvuta kamba, kukimbiza kuku, kukimbia na gunia, bao, draft, kukimbia mita 100 na mita 400 na kuendesha baiskeli mwendo wa polepole na karata.Washindi katika michezo hiyo watapatiwa kuku, vikombe na medali.
Mwenyekiti wa maandilizi ya Bonanza la Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzania (JMAT) Mhe. Jaji Shabani Lila akimkabidhi zawadi ya shukurani mgeni rasmi wa Bonanza hilo Mhe. Jaji Augustine Mwarija ambaye mi Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania na Mlezi wa Majaji wa Mahakama hiyo.
Mwakilishi wa timu ya mpira wa miguu timu ya Mahakama Kuu akionyesha kikombe cha ushindi wa mchezo wa mpira wa miguu alichokabidhiwa na mgeni rasmi.
Mwakilishi wa washindi wa timu ya mchezo wa kuvuta Kamba kwa wanaume akiwakilisha Mahakama ya Rufani walioshinda mchezo huo akionyesha kikombe cha ushindi alichokabidhiwa na mgeni rasmi.
Mwakilishi wa washindi wa timu ya mchezo wa kuvuta Kamba kwa wanawake akiwakilisha Mahakama Kuu akionyesha kikombe cha ushindi alichokabidhiwa na mgeni rasmi.
Mwakilishi wa team ya mpira wa Pete Mhe. Jaji Zahra Maruma ambaye ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kituo cha Usuluhishi akionyesha kikombe cha ushindi wa mchezo huo alichokabidhiwa na mgeni rasmi.
Mshindi wa mchezo wa Riadhaa Mita 400 Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe .Adelf Sachore akipewa mkono wa pongezi kutoka kwa mgeni rasmi kwa ushindi huo kwa upande wa wanaume.
Mshindi wa Mchezo wa Riadhaa mita 100 Bw Gishet Jental kutoka Mahakama Kuu akipewa mkono wa pongezi na Mgeni Rasmi kwa ushindi huo kwa wanaume.
Mshindi wa mashindano ya mchezo wa riadhaa mita mia na mita minne kwa upande wa wanawake , Bi. Grace Hamisi kutoka Mahakama Kuu Temeke akipewa mkono wa pongezi na mgeni rasmi kwa ushindi huo.
Mshindi wa mashindano ya kukimbia kwa Gunia kwa upande wa wanawake Bi Aziza Mete kutoka Mahakama Kuu Tanzania akipokea medali ya ushindi wa mchezo huo kutoka kwa mgeni rasmi.
Mshindi wa mashindano ya kukimbia kwa Gunia kwa upande wa wanaume Bw Hassan Chuka Mahakama ya Rufaa Tanzania akipokea medali ya ushindi kutoka kwa mgeni rasmi.
Mshindi wa mchezo wa bao kwa wanaume Bw Hashimu Rashid kutoka Mahakama Kuu Tanzania akipokea Medali ya ushindi wa mchezo huo kutoka kwa mgeni rasmi.
Mshindi wa mchezo wa bao kwa wanawake BI. Mwabibi Bakari kutoka Mahakama Kuu akipokea medali ya ushindi wa mchezo huo kutoka kwa mgeni rasmi.
Mshindi wa mchezo wa kuendesha baiskeli kwa mwendo wa polepole kwa upande wa wanaume, Jaji wa Mahakama ya Rufani Tanzania, Mhe. Sum Rumanyika akipokea medali.
Mshindi wa kukumbiza kuku, ambaye ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Yose Mlyambina akipewa mkono wa pongezi na mgeni rasmi.
Mwakilishi wa Ushindi mchezo wa karata upande wa wanawake Mahakama Kuu akivalishwa medali.
Mwakilishi wa ushindi wa mchezo wa karata upande wa wanaume.
Mshindi wa mchezo wa kuendesha baiskeli kwa mwendo wa polepole kwa upande wa wanawake, Mhe. Suzan Kihawa akipokea medali.
Mshindi wa kukumbiza kuku, upande wa Mahakama ya Rufani Tanzania, akipewa mkono wa pongezi na mgeni rasmi.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni