Na. Paul Paschal – Mahakama, Moshi
Uongozi na Watumishi wa Mahakma ya Hakimu Mkazi Moshi wamekutana na
kufanya kikao kazi cha mapitio ya kiutendaji ya mwezi septemba wenye lengo la
kuainisha mafanikio, changamoto na namna ya kuboresha utoaji huduma za
kimahakama kwa wananchi na wadau.
Akifungua kikao kazi
hicho kilichofanyika tarehe 29 Septemba, 2023 Hakimu Mkazi Mkuu Mfawidhi wa Mahakama
ya Hakimu Mkazi Moshi Mhe. Salome Mshasha alisema, aliwakumbusha
Watumishi wote kutambua dira ya Mahakama ni moja tu
kutoa haki kwa wananchi wote na kwa wakati, hivyo ni
vyema katumia maarifa na weledi kufanikisha hilo ni lazima kusimamia
misingi ya maadili, nidhamu na uwajibikaji.
Naye Afisa Tawala wa
Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi Bw. Paul Mushi alisema, Watumishi wanapaswa
kutunza na kusimamia rasilimali za ofisi ili kuwezesha kutimiza malengo ya
ofisi.
“tukiweza kuzimamia
rasilimali za ofisi yetu mambo yatakuwa mzauri na kuondoa changamoto. Pia
niwaombe kuongeza jitihada katika matumizi ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHEMA), vile vile tuhahikikishe taarifa za mashauri yote katika
kituo chetu zinauhishwa kwa wakati ili tuwe na taarifa sahihi za kiutendaji”.
aliongeza Afisa Tawala huyo.
Kwa upande wake
mtumishi wa Mahakama hiyo, Bw. Robert Cornel alisema, swala la
kutoa lugha nzuri kwa mtumishi anapo muhudumia mteja ni la msingi sana katika
utoaji haki, hii inajenga faraja kwa wateja hata pale ambapo maamuzi
yanakuwa hayajatolewa kwa upande wake na lugha nzuri daima
inapunguza malalamiko.
Kikao hicho hufanyika
kila mwisho wa mwezi kwa lengo la kufungua tathimini ya kiutendaji wa shughuli
za Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi sambamba na kuweka mipango kwa mwezi
unafuata.
Sehemu ya watumishi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Moshi wakifuatilia agenda za kikao kazi hicho cha tathimini cha mwezi Septemba.
(Habari Hii Imehaririwa na Innocent Kansha - Mahakama)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni