Alhamisi, 14 Septemba 2023

RAIS SAMIA AWAAPISHA MAJAJI WAPYA MAHAKAMA YA RUFANI, MAHAKAMA KUU

Na Mary Gwera-Mahakama

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan leo tarehe 14 Septemba, 2023 amewaapisha Majaji wanne wa Mahakama ya Rufani na wengine 20 kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Hafla fupi ya uapisho wa Majaji hao imefanyika Ikulu jijini Dar es Salaam huku ikihudhuriwa na Viongozi mbalimbali, akiwemo Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Dkt. Moses Kusiluka.

Viongozi wengine ni Majaji wa Mahakama ya Rufani, Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi, Jaji Kiongozi Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani, Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama, Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Albert Chalamila, Makamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama na Viongozi wengine.

Akizungumza mara baada ya uapisho, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Juma amemshukuru Rais Samia kwa kuendelea kuongeza nguvu kazi katika Mhimili huo.

“Uapisho wa Majaji hawa unaongeza idadi yao na kuwa na jumla ya Majaji 30 wa Mahakama ya Rufani na 105 wa Mahakama Kuu ya Tanzania,” amesema Mhe. Prof. Juma

Majaji wa Mahakama ya Rufani walioapishwa ni aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Kigoma, Mhe. Lameck Michael Mlacha na Mhe. Paul Joel Ngwembe ambaye alikuwa Jaji Mfawidhi Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Morogoro.

Wengine ni Mhe. Mustafa Kambona Ismail, aliyekuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi na Mhe. Abdul-Hakim Ameir Issa aliyekuwa Jaji wa Mahakama Kuu Zanzibar.

Majaji wa Mahakama Kuu ya walioapishwa katika hafla hiyo ni Mhe. Wilbert Martin Chuma, aliyekuwa Msajili Mkuu Mahakama ya Tanzania, Mhe. Sharmillah Said Sarwatt, aliyekuwa Msajili Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Evaristo Longopa, ambaye alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Wengine ni Bi. Sarah Duncan Mwaipopo, aliyekuwa Naibu Wakili Mkuu wa Serikali, Mhe. Anold John Kirekiano, aliyekuwa Naibu Msajili Mwandamizi Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Angelo Kataraiya Rumisha, aliyekuwa Naibu Msajili na Mkuu wa Kitengo cha Maboresho Mahakama ya Tanzania, Mhe. Said Rashid Ding’ohi, aliyekuwa Naibu Msajili Mwandamizi Mahakama Kuu, Divisheni ya Kazi, Mhe. Martha Mpaze, aliyekuwa Naibu Msajili Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia Temeke na Mhe. Ferdinand Hilali Kiwonde, aliyekuwa Naibu Msajili Mahakama Kuu.

Majaji wengine ni Bw. Ntuli Lutengano Mwakahesya, aliyekuwa Naibu Karani wa Baraza la Mawaziri, Ofisi ya Rais Ikulu, Dodoma, Bw. Griffin Venance Mwakapeje, aliyekuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Kurekebisha Sheria Wizara ya Katiba na Sheria Dodoma na Dkt. Dafina Daniel Ndumbaro, aliyekuwa Wakili wa Serikali Mwandamizi, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

Kwenye orodha yupo pia Bw. Emmanuel Ludovick Kawishe, aliyekuwa Mkurugenzi wa Huduma za Kisheria Tume ya Taifa ya Uchaguzi na Bw. Abdallah Halfan Gonzi, aliyekuwa Mjumbe wa Baraza la Rufani za Kodi na Mhadhiri Msaidizi Chuo Kikuu cha Dar es Salaama.

Wengine ni Bw. Kamazima Kafananbo Idd, aliyekuwa Mhadhiri Msaidizi Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) na Bw. Frank Muyoba Mirindo, aliyekuwa Mhadhiri Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA).

Pia wapo Bw. Hussein Salum Mtembwa, aliyekuwa Wakili wa Kujitegemea na Mmiliki wa Kampuni ya Uwakili ya HM NOBLE Attorneys, Mtwara, Bi. Aisha Ally Sinde, aliyekuwa Wakili wa Kujitegemea Kampuni ya Uwakili BOWMANS Tanzania, Bi. Irene Daniel Musokwa, aliyekuwa Wakili wa Kujitegemea na Mshiriki katika Kampuni ya Uwakili ya FC Attorneys na Bi. Hadija Ally Kinyaka, aliyekuwa Wakili wa Kujitegemea Kampuni ya Uwakili Lawhill 'Co. &Advocates'.

Katika hafla hiyo, Rais Samia amewaapisha pia Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki atakayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Balozi Stephen Patrick Mbundi, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Said Shaib Mussa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Balozi Prof. Kennedy Godfrey Gastorn.

Majaji wapya wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu ya Tanzania na Viongozi wengine wa Serikali wakila kiapo cha Maadili mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan (hayupo katika picha). Hafla ya uapisho imefanyika leo tarehe 14 Septemba, 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam.
Majaji wa Mahakama ya Rufani (waliosimama katikati) wakila kiapo cha maadili mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan (hayupo katika picha).
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Wilbert Chuma akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sharmillah Sarwatt akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Anorld Kirekiano akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Angelo Rumisha akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Said Ding'ohi  akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Martha Mpaze  akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Ferdinand Kiwonde  akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sarah Mwaipopo  akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. 

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Evaristo Longopa akila kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan. 
Sehemu ya Viongozi wa Serikali, Majaji wa Mahakama ya Rufani na wageni waalikwa wakiwa katika hafla ya Uapisho wa Majaji wapya wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu ya Tanzania walioapishwa leo tarehe 14 Septemba, 2023 Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan (katikati) akiwa katika picha pamoja na Majaji wapya wa Mahakama ya Rufani na Mahakama Kuu ya Tanzania (waliosimama ambao wamevaa majoho), wa tatu kushoto ni Waziri Mkuu wa Tanzania, Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa, wa pili kushoto ni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma, wa tatu kulia ni Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, wa pili kulia ni Jaji Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Khamis Ramadhan Abdalla, wa kwanza kulia ni Mhe. Sivangilwa Mwangesi, Kamishna wa Maadili, wa kwanza kushoto ni Katibu Mkuu Kiongozi, Mhe. Dkt. Moses Kusiluka. Waliosimama mstari wa mbele (waliovaa suti) wa (pili kulia) ni Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Dkt. Pindi Chana, (wa pili kushoto) ni Jaji Kiongozi Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Siyani, (kulia kwa Jaji Kiongozi) ni Mtendaji Mkuu Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel na (kushoto kwa Waziri wa Katiba na Sheria )ni Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria, Bi. Mary Makondo.
Walioketi mbele ni Majaji wapya wa Mahakama ya Rufani walioapishwa.
Sehemu ya Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania wakisubiri kuapishwa.

(Picha na Mary Gwera, Mahakama)






Hakuna maoni:

Chapisha Maoni