Na Faustine Kapama-Mahakama
Uamuzi wa Rais Samia Suluhu Hassan wa kumuongezea muda Prof. Ibrahim Hamis
Juma kuwa Jaji Mkuu wa Tanzania hauvunji Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania, kama ilivyofanyiwa marekebisho mara kwa mara.
Hii ni kufuatia uamuzi wa Mahakama Kuu, Masjala Kuu, uliotolewa jana tarehe
22 Septemba, 2023, na kutupilia mbali kesi ya kikatiba lililowasilishwa na
Humphrey Malenga, mleta maombi, ambaye ni raia wa kawaida.
“Rais ana mamlaka kwa mujibu wa Ibara ya 120 (3) inayosomwa pamoja na Ibara
ya 118 (2) ya Katiba ya kuongeza muda wa Jaji wa Rufani ili kumwezesha
kuendelea kutekeleza majukumu yake. Naona maombi hayana mashiko. Nayatupiliwa
mbali,” Jaji Godfrey Isaya alisema.
Katika maombi yake, mleta maombi alitaka amri ya kutafsiri masharti ya
Ibara ya 118 (2) ya Katiba kuhusu umri wa kustaafu wa Jaji Mkuu kuwa miaka 65
na si umri wa kustaafu kwa Jaji wa Rufani.
Pia alitaka tafsiri ya kifungu hicho kuwa ni Ibara inayosimama pekee na
haihusanishwi na masharti ya Ibara ya 120 (1) (2) (3) na (4) ya Katiba wakati
wa kuamua muda au umri wa kustaafu kwa Jaji Mkuu.
Aidha, mwombaji aliomba tafsiri ya mamlaka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano
wa Tanzania ya kusimamisha umri wa kustaafu wa Jaji wa Mahakama ya Rufani au
kuongeza muda wa utumishi wa Jaji wa Rufani kwa maslahi ya umma kwa mujibu wa
Ibara ya 120 (2) na (3) haimhusu Jaji wa Rufani ambaye pia ni Jaji Mkuu.
Alitaka pia tamko kwamba kusimamishwa kwa umri wa kustaafu au kuongeza muda
wa kukaa kwa Jaji wa sasa wa Rufani ambaye pia ni Jaji Mkuu, Prof. Ibrahim
Hamis Juma kwa mujibu wa kifungu cha 120 (2) na (30) ni kinyume cha Katiba.
Katika hukumu yake, Jaji Isaya alisema kuwa Ibara ya 118 ya Katiba haiwezi
kusomwa peke yake, bali inasomwa pamoja na Ibara ya 120 ya Katiba, hivyo
mamlaka ya Rais kuongeza muda wa Jaji Mkuu wa sasa madarakani yalikuwa sahihi,
hivyo yako sambamba na Katiba.
“Ibara ya 120 (1) haiwezi kusomwa kipekee na Ibara ya 120 (2) (3) na (4),
kwa maana hiyo kifungu cha 120 cha Katiba kinamhusu Jaji Mkuu, kusimamisha kwa
usahihi umri wa kustaafu au kuongeza muda wa Jaji wa Rufani ambaye ni Jaji Mkuu
kwa mujibu wa Ibara ya 120 (2) na (3) ni halali,” alisema.
Kabla ya kufikia uamuzi huo, Jaji Isaya alizingatia baadhi ya hoja kadhaa,
ikiemo iwapo Masharti ya Ibara ya 118(2) ya Katiba yanaruhusu umri wa kustaafu
wa Jaji Mkuu kuwa miaka 65 au umri wa kustaafu wa Jaji wa Rufani.
Jaji pia alizingatia iwapo Ibara ya 118(2) ya Katiba ni Ibara ya
"kusimama peke yake" wakati wa kuamua umri wa kustaafu wa Jaji Mkuu
wa Tanzania, au iwe katika kuamua umri wa kustaafu wa Jaji Mkuu wa Tanzania
kama ilivyoainishwa kwenye Ibara ya
118(2) ya Katiba inafanyiwa rejea kwenye Ibara ya 120(1) pekee na kutukuzingatia
masharti ya Ibara ya 120(2), (3) na (4) ya Katiba.
Pia ilizingatiwa iwapo mamlaka ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ya kusimamisha umri wa kustaafu kwa Jaji wa Mahakama ya Rufani au kuongeza muda
wa utumishi wa Jaji wa Mahakama ya Rufani kwa maslahi ya umma kwa mujibu wa
masharti ya Ibara ya 120 (2) na ( 3) ya Katiba ni sahihi.
Aidha, Jaji alizingatia iwapo kusimamishwa kwa umri wa kustaafu na/au
kuongeza muda wa kukaa kwa Jaji wa Mahakama ya Rufani ambaye ni Jaji Mkuu kwa
mujibu wa masharti ya Ibara ya 120(2) na, au 120(3) ya Katiba ya Jamhuri ya
Muungano. ya Tanzania kama ilivyofanyiwa marekebisho.
Katika kuamua hoja hizo, Jaji Isaya alieleza kuwa ni kweli maneno ya Ibara
ya 118(2) yametungwa kwa namna ambayo inamlazimu mtumishi wa ofisi ya Jaji Mkuu
kufanya kazi za utawala na Mahakama.
Alipata mantiki katika kutafsiri kwamba vifungu vilivyotajwa vinaunganisha
ofisi ya Jaji Mkuu na Jaji wa Rufani pamoja na kukubaliana na mwombaji kwamba
mwenye nafasi ya ofisi ya Jaji Mkuu pia ni Jaji wa Rufani.
“Sikubaliani na maoni ya mleta maombi kwamba kuna hatari na uvunjifu mkubwa
wa Katiba. Kabla ya kuteuliwa katika ofisi ya Jaji Mkuu, Jaji Mkuu aliyeko
madarakani alikuwa Jaji wa Rufani,” alisema.
Jaji Isaya aliuliza swali iwapo ibara ya 118 (2) ya Katiba inajitosheleza yenyewe
ndani ya Katiba. Alisema kuwa jibu la swali hilo ni hasi kwa sababu pande zote
mbili zinakubaliana kwamba umri unaotarajiwa wa kustaafu wa Jaji wa Rufani ni
kama ilivyoainishwa chini ya Ibara ya 120(1) ya Katiba.
“Hii ina maana, ili kupata umri wa kustaafu kwa Jaji Mkuu inabidi kufanya
marejeo ya Ibara ya 120(1) ya Katiba. Hii ni kwa sababu Ibara ya 118(2) ya
Katiba haiwezi kusimama yenyewe peke yake au inaweza kujitosheleza....
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni