TANZIA
Marehemu Alexander Simon Chandevu enzi za uhai wake.
TANZIA
Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Mtumishi wake Bw. Alexander Simon Chandevu aliyekuwa akihudumu kwa nafasi ya Mlinzi katika Mahakama ya Mwanzo Buguruni, Wilaya ya Ilala.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 12 Septemba, 2023 na Mtendaji wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Dar es Salaam-Kisutu, Bi. Athanasia Kabuyanja marehemu Chandevu alifikwa na umauti usiku wa kuamkia Jumamosi tarehe 09 Septemba, 2023 katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) alipokuwa akipatiwa matibabu.
Bi. Kabuyanja amesema maziko yalifanyika jana Jumatatu tarehe 11 Septemba, 2023, Chang'ombe Maduka Mawili, Temeke jijini Dar es Salaam.
Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki kuomboleza msiba huu wa kuondokewa na Mpendwa wetu.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni