Na Hasani Haufi – Mahakama, Songea.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Songea, Mhe. James Karayemaha
hivi karibuni amefanya ziara ya ukaguzi katika Mahakama za Wilaya na Mahakama
za Mwanzo mkoani Ruvuma.
Mhe.
Karayemaha alifanya ukaguzi katika Mahakama za Wilaya Nyasa, Mbinga, Namtumbo
na Tunduru pamoja na Mahakama za Mwanzo Namabengo, Luegu, Mkongo, Nakapanya,
Nandembo, Matemanga, Ndegu na Mbambabay na kutembelea ofisi ya Mkuu wa Wilaya
Tunduru.
Akiwa
katika Mahakama hizo, Mhe. Karayemaha alipokea taarifa ya utekelezaji wa
mashauri na utawala ambapo aliwapongeza watumishi wa Mahakama Kanda ya Songea
kwa jitihada zao katika utendaji kazi.
Alisema
kuwa jitihada hizo zimesaidia kiwango cha umalizaji wa mashauri kupanda kutoka
asilimia 96.5% hadi kufikia asilimia 98.5% katika kipindi cha robo ya
tatu ya mwaka
Sambamba
na hayo, Jaji Mfawidhi alisisitiza watumishi kuwa weredi, wafanisi, waadilifu
na wawajibikaji na wajitahidi kusoma, kuuelewa na kuuishi mpango mkakati wa
Mahakama.
“Kufanya
kazi kwa weredi, uadilifu na ufanisi sio ombi bali ni wajibu kwa kila mtumishi
wa umma, ili kufikia malengo ya taasisi mnapaswa kutekeleza majukumu yenu
kupitia misingi hiyo, pamoja na kusoma, kuuelewa na kuuishi mpango mkakati wa
Mahakama ili kuendana na mabadiliko yaliyomo ndani ya mpango huo, lengo ni
kupata matokeo chanya,” alisema.
Aidha,
Mhe. Karayemaha alisisitiza ushirikiano kitaaluma katika utendaji kazi na kwa watumishi
kujiunga kwenye vyama vya kitaaluma ili kuongeza weredi katika utendaji wao wa kazi.
“Kufikia
malengo ya taasisi kunahitaji watumishi kutekeleza majukumu mnayopewa kwa
ushirikiano, pia kwa lengo la kuongeza ufanisi na weredi mnapaswa kujiunga na
kushiriki kwenye vyama vya taaluma kwani mtapata mambo na mbinu mpya tofauti
tofauti ambazo zitakuongezea ujuzi,’’ alisema.
Viongozi wengine ambao aliambatana nao katika ziara hiyo Naibu Msajili wa Mahakama Kuu Kanda ya Songea, Mhe. Elizabeth Nyembele, Mtendaji wa Mahakama, Bw. Epaphras Tenganamba, Hakimu Mkazi Mfawidhi, Mahakama ya Hakimu Mkazi Songea, Mhe. Japhet Manyama na Msaidizi wa Sheria wa Jaji Mfawidhi Kanda ya Songea, Mhe. Lilian Haule.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Songea, Mhe. James Karayemaha akikagua
maeneo ya Mahakama ya Wilaya Mbinga.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Songea, Mhe. James Karayemaha akipokea
taarifa kutoka kwa Hakimu Mkazi Mfawidhi Mahakama ya Wilaya Mbinga (wa pili
kutoka kushoto).
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Songea, Mhe. James Karayemaha akisalimiana
na watumishi wa Mahakama ya Wilaya Mbinga.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Songea, Mhe. James Karayemaha akisalimiana
na watumishi Mahakama ya Wilaya Nyasa.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Songea, Mhe. James Karayemaha akisalimiana
na watumishi wa Mahakama ya Mwanzo Mkongo iliyopo Wilaya ya Namtumbo.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Songea, Mhe. James Karayemaha akitembezwa
eneo la mMhakama ya Mwanzo Namabengo iliyopo Namtumbo.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Songea, Mhe. James Karayemaha akipokea
taarifa kutoka kwa Hakimu Mkazi Mahakama ya Mwanzo Mbambabay (watatu kutoka
kushoto).
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Songea, Mhe. James Karayemaha akisalimiana
na watumishi wa Mahakama ya Wilaya Tunduru.
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Songea, Mhe. James Karayemaha akiwa
kwenye picha ya pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Tunduru (wa kwanza kutoka kulia
kwenye safu ya mbele).
Jaji
Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Songea, Mhe. James Karayemaha
akiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Mahakama ya Wilaya Namtumbo.
(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Iringa)
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni