Na. Paul Pascal –Mahakama, Moshi
Uongozi
wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Moshi kwa kushirikisha na wananchi wa
Kata ya Kilema Wilaya ya Moshi vijijini mkoani Kilimanjaro umeratibu zoezi la
ukarabati mkubwa wa jengo chakavu la Mahakama ya Mwanzo lililopo Kata hiyo ili
kuwezesha wananchi kupata huduma za kimahakama zilizositishwa toka mwaka 2018
kutokana na uchavu wa jengo hilo.
Akizungumza
katika kikao kilichofanyika hivi karibuni cha kuanzisha mchakato wa utekelezaji
wa ukarabati mkubwa wa jengo hilo, Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda
ya Moshi Bw. Donald Makawia alitoa rai kwa viongozi na wananchi wa Kata ya
Kilema kushirikiana bega kwa bega na kuunganisha nguvu kwa pamoja ili kurejesha
jengo hilo katika muonekano nadhifu na salama kwa ajili ya kuhakikisha wananchi
wanapata jengo bora la kutolea huduma ya haki.
“Itakubukwa
Mahakama hii ya kilema ilifungwa mwaka 2018 kutokana na uchakavu mkubwa hivyo
kushindwa kutumika kutolea huduma za kimahakama. Lakini mnamo mwaka 2023 Mahakama
hii iliweza kufunguliwa na kufanya shughuli zake kupitia jengo la kuazimwa
linalomilikiwa na Serikali ya Kijiji kutokana na uhitaji wa huduma za kimahakama”,
alisema Mtendaji huyo.
Mtendaji
Makawia alisema, ukarabati huo utajumuisha uvunjaji wa jengo la zamani, ujenzi
wa ukumbi wa wazi, ukarabati wa vyumba viwili vya waheshimiwa Mahakimu, ukarabati
wa chumba cha masijala, ukarabati wa chumba cha mahabusu pamoja na uwekaji wa
miundombinu ya maji na umeme.
Ukarabati
na ujenzi huo umetengewa kiasi cha fedha shilingi milioni 17 ambazo zimetolewa
toka Ofisi ya Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania (MMK - K) baada ya
kutembelea na kukagua Mahakama hiyo kwa maombi ya mtendaji wa mahakama kuu
kanda ya moshi mwezi augusti 2023. Aliongeza Bw. Makawia
Aidha,
Sambamba na mchango huo kutoka Ofisi ya Mtendaji wa Mahakama Kuu. Mahakama Kuu
Kanda ya Moshi imeungana na uongozi wa kata ya Kilema ikiwa ni utekelezaji wa
nguzo ya pili ya Mpango Mkakati wa Mahakama upatikanaji wa huduma za utoaji haki kwa wakati, maeneo
ya matokeo muhimu (ushirikishwaji wa wadau, majengo na miundo mbinu).
Ukarabati huo ulioanza kutekelezwa mnamo tarehe 10 Oktoba, 2023 na utafanywa kwa kutumia nguvu kazi ya wananchi na unatarajiwa kukamilika mwezi Novemba, 2023.
Hakuna maoni:
Chapisha Maoni