Ijumaa, 6 Oktoba 2023

MAHAKIMU MBEYA WAFUNDWA NA JMAT.

Mwinga Mpoli – Mahakama, Mbeya

Mahakimu Wakazi wa Mahakama ya Tanzania Mkoa wa Mbeya wamepatiwa mafunzo juu ya uandishi wa hukumu, uongozi pamoja na njia za ufundishaji.

Akizungumza hivi karibuni wakati wa mkutano wa Chama cha Majaji na Mahakimu Mkoa wa Mbeya (JMAT - Mbeya) uliofanyika wilayani Kyela Mkoa Mbeya. Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya Mhe. Dastan Ndunguru ambaye pia ni mlezi wa JMAT- Mbeya alisema kuwa, pamoja na muongozo unaoelekeza hukumu inatakiwa iweje mnatakiwa kuongeza utashi na kutumia lugha nyepesi inayoeleweka ili kuhakikisha mnatoa hukumu nzuri.

“Hukumu ni mawasiliano yaliyotokea Mahakamani kati ya wadaawa, na ili Hukumu iwe nzuri inahitaji kuwa na uhalisia, jambo ambalo linabishaniwa kisheria, na je jambo ilo linalingana na sheria husika? na mwisho kunahitajika hitimisho. Hapo tutapata hukumu yenye viwango na inayojitosheleza” alisema Mhe. Ndunguru.

Mhe. Ndunguru alitumia fursa hiyo mara baada ya  kufungua mafunzo hayo kwa kuunda kamati ndogo ndogo za ndani za maadili ya Mahakimu zitakazoongozwa na Waheshimiwa Majaji kwa lengo la kukumbushana na kuonyana ili kuhakikisha uadilifu na weledi unazingatiwa katika uendeshaji na utoaji wa huduma ya haki kwa wananchi.

Naye, Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Victoria Nongwa akizungumzia suala la uongozi alisema, uongozi ni jukumu na uongozi ni kipaji mtu alichojakliwa na Muumba.

“Kiongozi unatakiwa kuwatia moyo na kuwawezesha watu unaowaongoza, pia unatakiwa uwe na maono ya mbele, mbunifu na uwezo wa kutatua changamoto zinazojitokeza mbele yako” alisisitiza Mhe. Nongwa

Aidha, Jaji wa Mahakama ya Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. David Ngunyale ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya mafunzo na utafiti Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya alitoa mada ya namna ya kuandaa mafunzo na mikakati yake, pamoja na mazingira yatakayotumika kutoa mafunzo, alisema Mkufunzi anapaswa kujua njia ya ufundishaji atakayoitumia kwa walengwa wa mafunzo pamoja na gharama zake.

Meza Kuu ikiongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya Mhe. Dastan Ndunguru (wa tatu kulia walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mahakimu Wakazi wa Mahakama Mkoa wa Mbeya waliohudhuria mafunzo hayo.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. Dastan Ndunguru akifafanua jambo wakati wa mafunzo hayo kwa Mahakimu wakazi wa Mkoa wa Mbeya (hawapo pichani).

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Mbeya Mhe. David Ngunyale akitoa mada wakati wa mafunzo kwa Mahakimu hao (hawapo pichani).

Jaji wa Mahakama Kuu kanda ya Mbeya Mhe. Victoria Nongwa akitoa mada wakati wa mafunzo hayo kwa Mahakimu Wakazi hao (hawapo pichani)

Meza Kuu ikiongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya Mhe. Dastan Ndunguru (wa tatu kulia walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na Mahakimu Wakazi wa Mahakama Mkoa wa Mbeya waliohudhuria mafunzo hayo.

Meza Kuu ikiongozwa na Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Mbeya Mhe. Dastan Ndunguru (wa tatu kulia walioketi) akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya Mahakimu Wakazi wa Mahakama Mkoa wa Mbeya waliohudhuria mafunzo hayo.

(Habari Hii imehaririwa na Innocent Kansha - Mahakama)


Hakuna maoni:

Chapisha Maoni