Jumamosi, 7 Oktoba 2023

MENEJIMENTI KUU YA MAHAKAMA YA TANZANIA YAKUTANA MOROGORO

Na Evelina Odemba – Mahakama Morogoro

Menejimenti Kuu ya Mahakama ya Tanzania imekutana mkoani hapa leo tarehe 7 Oktoba, 2023, kujadili masuala mbalimbali ya msingi ya kiutendaji.

Katika kikao hicho, Mwenyekiti wake ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel alisisitiza kuendelea kuboresha huduma za upatikanaji wa haki kwa wananchi.

Menejimenti hiyo inaundwa na wakuu wa idara na vitengo vyote ndani ya Mahakama ya Tanzania, huku Mwenyekiti Mwenza akiwa ni Msajili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Sylvester Kainda.

Kwa upande wake, Mhe. Kainda alizungumzia suala la mashauri na kueleza kuwa Mahakama ya Rufani imeboresha utoaji wa takwimu tofauti na ilivyokuwa miaka ya nyuma.

Kikao hicho pia kilipokea taarifa mbalimbali za uwajibikaji ambazo zimefanyiwa kazi kama ilivyoazimiwa na kikao kilichopita. Taarifa hiyo ilisomwa na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mahakama ya Tanzania, Bi. Beatrice Patrick.

Mahakama ya Tanzania, kupitia mpango mkakati wake, imejikita katika uboreshaji wa huduma mbalimbali, ikiwemo majengo. Miongoni mwa maboresho hayo ni uwepo wa Vituo Jumuishi vya Utoaji Haki (IJCs).

Mwenyekiti wa kikao cha Menejimenti Kuu ya Mahakama ya Tanzania, ambaye pia ni Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel akiendesha kikao. Kushoto ni Mwenyekiti Mwenza ambaye ni Msajili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Sylvester Kainda.

Viongozi wa Menejimenti Kuu ya Mahakama ya Tanzania, akiwemo Mwenyekiti wa Kikao ambaye ni Mtendaji Makuu wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabrie (katikati), Mwenyekiti Mwenza, ambaye ni Msajili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Sylvester Kainda (kulia) na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Mahakama ya Tanzania, Bi. Beatrice Patrick, wakifuatilia yaliyokuwa yanajiri kwenye kikao.

Wajumbe wa kikao cha Menejimenti Kuu ya Mahakama wakipiga makofi wakati Katibu wa Kikao, Bi. Beatrice Patrick (aliyesimama mbele) akiwapitisha katika taarifa fupi ya masuala yaliyotekelezwa na Mahakama ya Tanzania pamoja na mrejesho wa taarifa ya kikao kilichopita.

Mjumbe wa kikao cha Menejimenti Kuu ya Mahakama ya Tanzania akichangia hoja.

Mwenyekiti Mwenza wa Kikao cha Menejimenti Kuu ya Mahakama ya Tanzania, ambaye pia ni Msajili wa Mahakama ya Rufani, Mhe. Sylivester Kainda akifuatilia kinachoendelea kwenye kikao.

Katibu wa Kikao cha Menejimenti Kuu ya Mahakama ya Tanzania, Bi. Beatrice Patrick akichangia mada wakati wa kikao.

Sekretarieti ya Kikao cha Menejimenti Kuu ya Mahakama ya Tanzania wakati wa kikao.

Sehemu ya wajumbe wa Menejimenti Kuu ya Mahakama ya Tanzania ikiwa katika kikao.

Mjumbe wa Menejimenti Kuu ya Mahakama ya Tanzania akichangia mada.

(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Iringa)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni