Jumapili, 29 Oktoba 2023

TANZIA; MTUMISHI MAHAKAMA YA WILAYA KARATU AFARIKI DUNIA

TANZIA

Bw. Kayugi Daudi Mlekwa enzi za uhai wake.

Mahakama ya Tanzania inasikitika kutangaza kifo cha aliyekuwa Mtumishi wake Bw. Kayugi Daudi Mlekwa aliyekuwa akihudumu kwa nafasi ya Dereva Daraja la II Mahakama ya Wilaya Karatu mkoani Arusha.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo tarehe 29 Oktoba, 2023 na Mtendaji Mahakama Kuu Arusha, Bw. Leonard Maufi marehemu Mlekwa alifikwa na umauti tarehe 27 Oktoba mwaka huu alipokuwa akicheza mpira wa kikapu 'basket ball' ambapo alianguka ghafla na kufariki papo hapo.

Bw. Maufi amesema mipango ya maziko inafanyika, ambapo kwa sasa wamepanga kuusafirisha mwili wa marehemu Mlekwa kwenda mkoani Mwanza kesho tarehe 30 Oktoba, 2023. 

Mazishi ya marehemu Mlekwa yatafanyika Siku ya Jumanne tarehe 31 Oktoba mwaka huu Kirumba mkoani Mwanza.

Mahakama ya Tanzania inaungana na ndugu, jamaa na marafiki kuomboleza msiba huu wa kuondokewa na Mpendwa wetu.

BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA, JINA LAKE LIHIMIDIWE.

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni