Jumatatu, 2 Oktoba 2023

WATUMISHI WAPYA WA MAHAKAMA KUU DIVISHENI WAASWA KUZINGATIA KIAPO NA SIRI

 Na Magreth Kinabo- Mahakama

 

Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Biashara, Bw.Edward Mbara amewataka watumishi wa ajira mpya kutoka katika Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni mbalimbali kuzingatia mafunzo ya utunzaji wa nyaraka na kiapo cha kutunza siri Serikalini kwa kuwa ni suala muhimu katika Utumishi wa Umma.

 

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo, yaliyofanyika tarehe 02 Oktoba, 2023 kwenye ukumbi wa mkutano wa Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia (TMK) kilichopo jijini Dar es Salaam, ambapo aliwaomba kutoa taarifa sahihi za watu wa karibu hususan watakaotoa mawasiliano yao ili iwe rahisi kutafutwa wakati wowote pindi taarifa za mtumishi zinapotakiwa.

 

“Ninawaomba muwe watii katika kutekeleza majukumu yenu kwenhye Utumishi wa Umma, ikiwa ni Pamoja na kufuata taratibu za kazi. Mafunzo hayo yatasaidia mtumishi kujua nini anatakiwa kufanyana nini hatakiwi kufanya ili siku zote asije kusema hakuelezwa au kufundishwa,” amesema Bw. Mbara.

 

Kwa upande wake Wakili wa Serikali Mkuu kutoka katika Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Nchini (DPP), Jenipher Massue aliwataka watumishi hao,kuzingatia Sheria ya Usalama wa Nchi ya 1970 na kuishi kulingana na viapo vyao.

 

Kwa upande wake Mtendaji wa Kituo cha Jumuishi cha Masuala ya Familia (TMK), Bw.Samson Mashalla aliwaasa watumishi hao, wakati akifunga mafunzo hayo kuwa  kujiendeleza kielimu ili waweze kufikia ngazi mbalimbali ikiwemo Ujaji.

 

Watumishi hao 31 wa kada tofauti wanatoka Divisheni za Biashara, Ardhi,Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Kazi, Kituo cha Usuluhishi na Kituo Jumuishi cha Masuala ya Familia (TMK).

 

Watumishi hao, wakila kiapo cha   Maadili ya Utumishi wa Umma.

 


Mtendaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Biashara, Bw. Edward Mbara akizungumza na watumishi  wa ajira mpya kutoka katika  Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni mbalimbali.

Wakili wa Serikali Mkuu kutoka katika Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Nchini(DPP), Jenipher Massue akitoa maelezo kuhusu ujazaji wa fomu ya kiapo cha  Maadili ya Utumishi wa Umma kwa watumishi hao.

Afisa Utumishi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Biashara, Bi. Fadhilina Mdee akitoa neno la utangulizi kwenye mafunzo hayo.

Watumishi hao, wakijaza fomu ya Maadili ya Utumishi wa Umma.

Watumishi hao, wakijaza fomu ya maelezo binafsi.

 Mtendaji wa Kituo cha Jumuishi cha Masuala ya Familia (TMK), Bw.Samson  Mashalla akifunga mafunzo hayo.

 

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni