Jumatano, 22 Novemba 2023

BARAZA LAKAGUA VYUO VIKUU VINAVYOTOA ELIMU YA SHERIA MOSHI, ARUSHA

Na Brian Haule-Afisa UtumishiMahakama Kuu Masjala Kuu

Mwenyekiti wa Baraza la Elimu ya Sheria nchini, ambaye pia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani ameliongoza Baraza hilo kufanya ziara ya ukaguzi wa Vyuo Vikuu vinavyotoa elimu ya Sheria katika Mikoa ya Moshi na Arusha.

Ukaguzi huo ulianza tarehe 20 Novemba, 2023 kwa upande wa Vyuo Vikuu vya Mwenge Catholic University (MWECAU) na Moshi Co-Operative University (MoCU), tarehe 21 Novemba, 2023 ukaguzi umefanyika katika Chuo Kikuu cha Tumaini Makumira Arusha na kwa upande wa tarehe 22 Novemba, ukaguzi umefanyika katika Chuo Kikuu cha SAUT -Arusha.

Akiongea katika kaguzi hizoMhe. Siyani alisema lengo kuu la Baraza la Elimu ya Sheria ni kusimamia ubora wa elimu ya Sheria nchini, hivyo kaguzi hizo zitasaidia kufanya maboresho ya ubora wa elimu unaotakiwa kutolewa na Vyuo hivyo kwa Wanafunzi wanasomea fani hiyo.

Baraza la Elimu la Sheria likiongozwa na Mwenyekiti wake, limefanikiwa kufanya ukaguzi katika maeneo mbalimbali, ikiwemo miundombinu (majengo), idadi ya Walimu wanaofundisha katika Vyuo hivyo na sifa za Walimu wanaohitajika kufundisha Vyuo Vikuu.

Maeneo mengine yaliyokaguliwa ni maktaba za Vyuo, kama kuna vitabu vya kutosha na vya kisasa, matumizi ya Online kwa wanafunzi katika kutafuta vitabu kwa ajili ya kujisomea, namna ya utungaji wa mitihani ya Sheria kwa Wanafunzi, ofisi za Walimu Vyuoni na mabweni ya Wanafunzi.

Baada ya kuangalia katika maeneo hayo, Baraza liliwasilisha mapendekezo kadhaa, ikiwemo Vyuo Vikuu husika kuhakikisha inakuwa na miundombinu rafiki kwa kuhakikisha majengo yanakuwa katika hali nzuri na maboresho katika majengo hayo yazingatie kujenga sehemu kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu.

Pia idadi ya Walimu iwe ya kutosha kwa ajili ya kuwa na uwiano sahihi kulingana na wanafunzi waliopoVyuo Vikuu husika vizingatie sifa za walimu wanaostahili kufundisha Chuo Kikuu wakati wanapotoa ajira na maktaba za Vyuo husika ziboreshwe kwa kuhakikisha kunakuwa na mazingira rafiki ya kusomea, vitabu vya kutosha na Vitabu vya Kisasa.

Kadhalika, Baraza limependekeza Vyuo vihakikishe vinawahimiza wanafunzi katika Matumizi ya Online wakati wa kujisomea, utungaji wa mitiahi uzingatie viwango vya juu katika kupima uelewa wa wanafunziVyuo vihakikishe Mabweni ya Wanafunzi yanakuwa katika hali nzuriVyuo vihakikishe walimu au watumishi wanakaa katika Ofisi yenye mazingira mazuri na vihakikishe mabweni yanakuwa yakutosha na katika hali nzuri.

Aidha Mhe. Mwenyekiti wa Baraza amewaasa wanafunzi wa Vyuo Vikuu husika kujituma na kuongeza juhudi binafsi wakati wanapokuwa Chuoni na kuachana na masuala ya starehe ambayo kwa sasa hayana faida katika masomo yao.

“Someni mkijiandaa vizuri mtafaulu vizuri, kila kitu ukitaka kupata lazima uwe na nidhamu, kwani kwenye bidii ndio Mungu husaidia watu,alisema akiwa katika Chuo Kikuu MoCU.

Katika Ziara hiyo, Mwenyekiti wa Baraza la Sheria Nchini aliambatana na Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Arnold John KerekianoKaimu Msajili  wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Projestus Kahyoza na Mhadhiri wa Chuo Kikuu Dar es Salaam, Dkt. Erasmo Nyika.

Wengine ni Wakili Mwandamizi, Msomi Silwan Galati, Bi. Frida Mwera kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali), Dkt. Lugaziya Mutabaazi, ambaye ni Mwakilishi kutoka Chama cha Mawakili Tanganyika na Sekretarieti inayojumisha Christina Mlwilo (JLA), Bi. Aneth Lyimo (MMO) na Brian Haule (HRO).

Ziara hiyo imehitimishwa leo tarehe 22 Novemba, 2023 katika Chuo cha Mtakatifu Augustino. (SAUT).


Mwenyekiti wa Baraza la Elimu ya Sheria nchini, ambaye pia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Chuo Kikuu cha MWECAU-Moshi.

Mwenyekiti wa Baraza la Elimu ya Sheria nchini, ambaye pia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani akisaini kitabu cha wageni katika Ofisi ya Mkuu wa Chuo cha MWECAU Moshi.

Mwenyekiti wa Baraza la Elimu ya Sheria nchini, ambaye pia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani akifanya ukaguzi wa vitabu vilivyopo katika Maktaba ya Chuo Kikuu MWECAU-Moshi, wengine ni wajumbe wa Baraza hilo.

Mwenyekiti wa Baraza la Elimu ya Sheria nchini, ambaye pia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani akiwa pamoja na baadhi ya wajumbe akikagua mfumo wa online library katika Chuo Kikuu cha MWECAU Moshi.

Picha ikimuonesha Mwenyekiti wa Baraza la Elimu ya Sheria nchini, ambaye pia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani (katikati waliokaa), pamoja na wajumbe wa Baraza ,wa kwanza kutoka kulia ni Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Arnold Kerekiano, Dkt. Erasmo Nyika na Frida Mwera, wa pili kutoka kushoto ni Silwani Galati, wa tatu kutoka kushoto ni Dkt. Lugaziya Mutabaazi na wa kwanza kushoto ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha MWECAU.

Baadhi ya Wanafunzi wa Chuo Kikuu MWECAU MOSHI wakiwa wanafuatilia maelekezo darasani.

Mwenyekiti wa Baraza la Elimu ya Sheria nchini, ambaye pia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani Mwenyekiti wa Baraza la Elimu ya Sheria nchini, ambaye pia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani akipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Idara ya Sheria wa Chuo Kikuu MoCU-Moshi.

Mwenyekiti wa Baraza la Elimu ya Sheria nchini, ambaye pia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani (katikati) akipata maelezo kutoka kwa Mkutubi wa Chuo Kikuu MoCU.

Mwenyekiti wa Baraza la Elimu ya Sheria nchini, ambaye pia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani (katikati mbele) akiwa katika Kikao na wajumbe pamoja na Viongozi wa Chuo Kikuu Tumaini Makumira-Arusha.

Mwenyekiti wa Baraza la Elimu ya Sheria nchini, ambaye pia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani (katikati) akikagua sehemu ya Ofisi ya Chuo Kikuu SAUT Arusha, wa pili kushoto ni Mwalimu wa Chuo Kikuu SAUT – ARUSHA.

Mkuu wa Chuo cha SAUT Arusha (aliyesimama) akiwa anatoa maelezo huku Mwenyekiti wa Baraza la Elimu ya Sheria nchini, ambaye pia ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani (mbele katiakati) pamoja na wajumbe wakiwa wanamsikiliza.

(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni