Alhamisi, 23 Novemba 2023

MAJAJI WAPYA RAHA SANA

  •    Wawili Dodoma wamaliza mashauri 65 ndani ya mwezi
  •    Kasi hiyo yawaibua wadau, wasema kipele kimepata mkunaji

Na Arapha Rusheke-Mahakama Kuu, Dodoma 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan mwezi Septemba, 2023 aliteua Majaji wanne wa Mahakama ya Rufani na wengine 20 kuwa Majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

Baada ya kuapishwa siku 10 baadaye, Mahakama ya Tanzania iliwapeleka Majaji hao kwenye Chuo cha Mahakama Lushoto kwa ajili ya ‘kuwanoa’ ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu watakapoanza kazi za kuwatumikia Watanzania kwa dhamana waliyopewa.

Majaji hao walikaa IJA kwa takribani wiki tatu na baadaye kupangwa kwenye vituo vya muda kusikiliza mashauri mbalimbali. Miongoni mwa Majaji hao, ni Mhe. Sharmillah Sarwatt na Mhe. Dkt. Evarist Longopa ambao walipangiwa katika kituo cha Dodoma.

Baada ya kuwasili katika kituo hicho, Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Dkt. Juliana Massabo aliwapokea kwa ukarimu na kuwaomba waanze kuchapa kazi. 

Walichokifanya Majaji hao wawili ndani ya mwezi mmoja kimewashangaza wengi, kwani wamefanikiwa kumaliza mashauri 65 na hakuna kiporo chochote walichokiacha kabla ya kuitwa na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Mustapher Mohamed Siyani kwenda kuhudumu katika vituo vingine.

Katika hafla fupi ya kuwashukuru iliyofanyika tarehe 21 Novemba, 2023 kwenye ukumbi wa mikutano katika Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Dodoma, Jaji Mfawidhi aliwapongeza Majaji hao kwa kazi nzuri waliyofanya tangu walipoanza kusikilizz mashauri hayo kuanzia tarehe 23 Octoba, 2023 hadi tarehe 21 Novemba, 2023.

 “Niwapongeze sana Majaji wetu kwa kazi nzuri na kubwa mliyoifanya hapa Dodoma ndani ya siku 28, lakini pia kwa ushirikiano wenu kipindi chote mlichokuwa nasi hapa, tunawashukuru na hongereni sana. Tunawatakia kheri katika vituo vyenu mlivyopangiwa,” Mhe. Dkt. Massabo alisema.

Kwa upande wao, Majaji hao walitoa shukrani zao kwa ushirikiano walioupata tangu walipowasili Dodoma.  Waliwashukuru pia kwa upendo uliopo Dodoma kuanzia kwa  Majaji hadi watumishi wa ngazi zote bila kujali vyeo vyao.

Halfa hiyo ya kuwapongeza Majaji hao ilihudhuriwa na Majaji, Mahakimu na watumishi wengine wa Mahakama Mkoa wa Dodoma.

Kasi hiyo ya kusikiliza mashauri iliyoonyeshwa na Mhe. Sarwatt na Mhe. Dkt. Longopa imewaibua wadau ambao wamempongeza Rais Samia kwa kuteua Majaji wachapaka kazi na wenye weledi mkubwa wanaojali maslahi ya Watanzania. 

Kadhalika, wamemshukuru Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma kwa uongozi na usimamizi mzuri unaowawezesha Majaji kutekeleza majukumu yao kwa uhuru na ufanisi wa hali ya juu.

“Mimi binafsi nimepata faraja kubwa sana kuona Majaji wetu wanafanya kazi kwa kujituma kiasi hiki. Kama hawa Majaji wawili tu wamefanikiwa kumaliza mashauri 65 kwa mwezi, kwa hao wengine 18 hali ikoje, kweli Mama ametuletea majembe,” Mkazi mmoja wa Dodoma aliyejitambulisha kwa jina la Bakari Msulwa alisema.

Mdau wa Mahakama ambaye hakupenda jina lake litajwe amesema kazi iliyofanywa na Majaji hao haina budi kupongezwa na anaamini mlundikano wa mashauri mahakamani utakuwa historia kama Majaji wapya wataunganisha nguvu na wale waliopo kwa sasa.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sharmillah Sarwatt akıla kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Evarist Longopa akıla kiapo mbele ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan.

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma(aliyesimama) akizungumza jambo wakati akifungua hafla ya kuwapongeza Majaji wapya waliokuwa wanahudumu katika Kanda yake kwa muda baada ya kutoka kwenye mafunzo Lushoto.

Majaji wapya wakikata keki kwa furaha, kushoto ni Mhe. Sharmillah Sarwatt na kulia ni Mhe. Dkt. Evarist Longopa.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Sharmillah Sarwatt (aliyesimama) akitoa neno la shukrani kwa watumishi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Dodoma.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Evarist Longopa (aliyesimama) akitoa neno la shukrani kwa watumishi wa Kituo Jumuishi cha Utoaji Haki Dodoma

Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dodoma, Mhe. Dkt. Juliana Massabo akisema neno la shukrani katika hafla ya kuwapongeza Majaji hao.

(Habari hii imehaririwa na FAUSTINE KAPAMA-Mahakama, Dar es Salaam)

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni