Alhamisi, 23 Novemba 2023

JMAT DAR, WATUMISHI WA MAHAKAMA KUTOA MSAADA KWA WAHITAJI

 Na Magreth Kinabo- Mahakamas

 

Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzanua (JMAT) Tawi la Dar es Salaam, Mhe. Shabani Lila,   amewahimiza  Viongozi na wanachama  tawi hilo, wakiwemo watumishi wengine  wa mkoa huo,   kujitokeza kwa  ajili ya  kuwatembelea na kutoa sadaka  kwa watu wenye mahitaji maalum, katika tukio litakalofanyika  Siku ya  Jumapili  ya tarehe 26 Novemba,. 2023. 

 

 Akizungumza katika kikao kilichofanyika tarehe 22 Novemba, 2023, kwenye ukumbi  Namba  Moja  wa Mahakama ya Rufani Tanzania, uliopo  jijini Dar es Salaam, Mhe. Jaji Lila, ambaye ni Mlezi wa tawi hilo, alisema  matendo  hayo ni ibada, hivyo wanachama wote na watumishi  wanaalikwa ili kufanikisha tukio hilo.

 

 Mhe. Jaji Lila, ambaye pia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Tan zania, amesema katika matendo  hayo watu wenye mahitaji maalum ambao ni watumishi wa Mahakama  watapatiwa fedha kwa ajili ya kuwawezesha kuendelea  kujikimu. Pia msaada wa vitu mbalimbali, hutatolewa kwenye  Kituo cha kulea watoto wenye mahitaji maalumu  cha Mburahati ili kuwafanya wajisikie faraja.

 

“Katika tukio hili tutafanya kazi nao na kula chakula cha mchana  pamoja ili kuwafanya wajisikie wako na walezi wao.” alisema  Mwenyekiti huyo.

 

Aidha Mhe. Lila amasema sehemu ya kukutana kwa ajili ya matendo hayo itakuwa ni eneo la Mahakama ya Rufani  na Mahakama Kuu ya  Tanzania Dar es Salaam, kuanzia saa 3: 00 asubuhi, ambapo usafiri wa pamoja  utakuwepo ili kuwawezesha  watumishi kufika kwenye maeneo ya wahitaji hao kuanzia saa 4.00 asubuhi. Imehimizwa kwenye Kikao hicho, kila mshiriki kuwasili katika eneo la safari hiyo akiwa na hitaji lolote kwa ajili ya wahitaji. Kikao kiliazimia kuwa vazi la siku hiyo kuwa ni tisheti za JMAT aina yoyote ya Mahakama ya Tanzania.

 

Kwa upande wake, Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya   matukio hayo, ambaye ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Yose Mlyambina alivitaja vitu vitakavyotolewa kwa watoto hao, kuwa ni michango ya vyumba vya kulala, magodoro, vyandarua,vitanda, mashuka, vikiwemo  vitu mbalimbali  vya matumizi ya nyumbani kama vile sabuni, mafuta, dawa za meno, nguo za aina mbalimbali.

 

Vitu vingine ni ada za shule na vyakula vya aina yoyote, taulo za kike na za watoto.


Mwenyekiti wa Chama cha Majaji na Mahakimu Tanzanua (JMAT) Tawi la Dar es Salaam, Mhe. Shabani Lila(kushoto),   amewahimiza  Viongozi na wanachama  tawi hilo, wakiwemo watumishi wengine  wa mkoa huo,   kujitokeza kwa  ajili ya  kuwatembelea na kutoa sadaka  kwa watu wenye mahitaji maalum, katika tukio litakalofanyika  Siku ya  Jumapili  ya tarehe 26 Novemba,. 2023.Kulia ni  Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya   matukio hayo, ambaye ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Yose Mlyambina.

Katibu wa Kamati ya Maandalizi ya   matukio hayo, ambaye ni Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Kazi, Mhe. Dkt. Yose Mlyambina(Kulia) alivitaja vitu vitakavyotolewa kwa wahitaji hao.

 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Bi. Mary Shirima akiwa katika kikao hicho. Wengine ni wajumbe wa kikao  hicho.

Sekretatrieti ya kikao hicho. 

 

 

 

 

 

Hakuna maoni:

Chapisha Maoni